LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 15, 2021

KIWANDA CHA GF VEHICLES ASSEMBLERS CHAKAMILISHA MAGARI 100, CHAOMBA SERIKALIA KUINGIZA NCHINI MAGARI YASIYOUNGANISHWA ILI KUUNGANISHWA NA VIWANDA VYA TANZANIA

Meneja Mkuu wa Kiwanda cha kutengeneza Magari mapya cha Kwanza nchini Tanzania GF- Vehicle Assembly Ltd , Ezra Mereng, akizungumza na wateja wa Kiwanda hicho kilichopo Kibaha mkoa wa Pwani, wakati wa sherehe ya kukamilisha magari 100 leo, yaliotengenezwa na kiwanda hicho kwa kipindi Cha miezi nne.

Baadhi ya magari yaliyounganishwa katika kiwanda hicho.

Wafanyakazi wa kiwanda hicho wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa sherehe hiyo, leo.

……………

 Kibaha, Pwani

Kiwanda kipya na cha kwanza cha kutengeneza na kuunganisha magari nchini Tanzania GF cha Vehicles Assemblers (GFA) kilichopo Kibaha katika mkoa wa Pwani leo kimetimiza utengenezaji gari la mwisho kukamilisha utengenezaji wa magari100 ulioanza mwezi Januari hadi mwezi huu wa Aprili mwaka huu.

Akizungumza wakati wa sherehe za kuruhusu gari ya 100 kukanyaga aridhini baada ya kuunganishwa tayari kwa kwa kutembea, Meneja Mkuu wa Kiwanda cha hicho, Ezra Mereng alisema ni kazi ngumu kukamilisha zoezi la uunganishaji na utengenezaji wa magari hayo kwa kuwa Tnzania ndio kiwanda cha kwanza kutengeneza (kuunganisha) magari.

"Changamoto ni nyingi kutokana na kutokuwa na wataalamu wengi katika sekta hii ya Magari lakini kwa kushirikiana na wataalamu wa nje tuliweza kuunganisha magari 100 ya awali na baadae wao wakaondoka na tukabaki na watanzani wenzetu ambao kwa uwezo wa Mungu leo tumefanikiwa kumaliza gari ya 100.

Mereng ameziomba Tasisisi za serikali kuagiza magari ambayo hayajaunganishwa ili kazi ya kuunganisha ifanyiwe na viwanda vya ndani ili kukuza pato la taifa na kuweza kuongeza ajira kwa Watanzania na pia nchi ijipatie fedha za kikgeni kwa kuuza nchi jirani magari yanayotoka Tanzania.

Nae afisa masoko na manunuzai wa kampuni ya uuzaji wa magari ya FG Trucks & Equipments Ltd , Hamis Hasasn ambao ni moja ya wateja waliopeleka kazi ya kuunganishiwa magari yao katika kiwanda hicho amesema, mwanzo wateja walikua hawaamini kama magari hayo yatakuwa na ubora, lakini kwa kipindi hiki magari yapo mitaani na yanafanya vizuri.

Kiwanda hicho kimeajiri Wafanyakazi 100 ambao ni pamoja wenye ajira za kudumi mikataba pamoja na za muda mfupi.

1 comment:

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages