Apr 18, 2020

KUANZIA JUMATATU KILA MTU AVAE MASK

  Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda ameagiza kuwa mtu yeyote anayeenda katika eneo lolote la manunuzi lazima awe amevaa Barakoa (mask)

Amesema haijalishi ila lazima watu wavae Barakoa “Ununue, ukate kanga, ukate leso na utafute rubber bands. Lazima uwe umevaa Barakoa”


Aidha, ameagiza kuwa kuanzia Jumatatu biashara zote zifanyike kwa mfumo wa ‘take away’ yaani ufike sehemu ya kununua bidhaa, nunua na ondoka

Pia, amewataka watu kuhakikisha wanakaa umbali wa mita 2 kila wakiwa eneo la msongamano wa watu huku akiwataka wenye masoko kutafuta mfumo mbadala na mzuri wa kusimama sokoni

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Pages