Rais Dk. John Magufuli akitoa salam katika Ibada ya Jumapili, iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Paulo wa Msalaba, Jimbo Kuu la Kanisa Katoliki la Dodoma. jijini Dodoma, leo.
DODOMA, Tanzania
Rais Dk. John Magufuli amewataka Watanzania kutotishwa na janga la ugonjwa wa homa ya mapafu inayosababishwa na virusi vya Corona, badala yake waendelee kufanya kazi kwa bidii na kujenga uchumi huku wakizingatia tahadhari zote za kujikinga kuambukizwa ugonjwa huo kama zilivyotolewa na wataalamu.
Rais Magufuli amesema hayo leo, Machi 22, 2020 alipohudhuria Ibada ya Jumapili katika Kanisa la Mtakatifu Paulo wa Msalaba, Jimbo Kuu la Kanisa Katoliki la Dodoma, iliyoongozwa na Paroko wa Parokia hiyo Padre Onesmo Wisi.
Katika salamu zake katika Ibada hiyo, Rais Magufuli amesema kuwepo kwa ugonjwa wa Corona isiwe sababu ya kutishana kiasi cha kumsahau Mwenyezi Mungu, hivyo ametoa mwito kwa Wakristo na Waumini wa madhehebu mengine kumrudia Mwenyezi Mungu ili aepusha janga hili, badala ya kumwacha shetani atawale.
Rais Magufuli amekemea tabia za baadhi ya watu wanaofanya mzaha juu ya ugonjwa huu ama kuwatia hofu wananchi kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.
“Watu tusitishane, tunatishana mno. Niwaombe ndugu Wakristo na Watanzania kwa ujumla wa Madhehebu yote, huu ndio wakati mzuri sana wa kumtegemea Mungu kuliko wakati wote, tuendelee kuchapa kazi, tuendelee kuujenga uchumi wetu, hatuwezi kusalimu amri kwa ugonjwa huu wa Corona na kushindwa kumtegemea Mungu na tukashindwa kuendeleza uchumi wetu” amesema Rais Magufuli.
Amewashukuru viongozi wa Dini kwa kuungana na Serikali katika kuwahamasisha wananchi kuchukua tahadhari na ametoa wito kwa viongozi hao kuendelea kuliombea Taifa ili Mwenyezi Mungu aepushe balaa la Corona.
Mar 22, 2020
Home
Corona
featured
RAIS DK. MAGUFULI AWATAKA WATANZANIA WASITISHWE NA JANGA LA CORONA, WAENDELEE KUCHAPA KAZI HUKU WAKIZINGATIA TU TAHADHARI ZOTE ZA KUJIKINGA NA UGONJWA HUO
RAIS DK. MAGUFULI AWATAKA WATANZANIA WASITISHWE NA JANGA LA CORONA, WAENDELEE KUCHAPA KAZI HUKU WAKIZINGATIA TU TAHADHARI ZOTE ZA KUJIKINGA NA UGONJWA HUO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Asante saana baba yetu,Rais wetu mpendwa ulioyatamka yote NI mema tupo pamoja,km ulivyosisitiza hili NI janga lkn tumuweke mungu mbele,hakika sisi sote NI waja wake,kujikinga na kufuata maelekezo tunayopewa ni wajibu wetu,lkn tusisahau MUNGU ananafasi ya pekee,hivyo tufanye kazi zetu km kawaida, tupo pamoja mh Rais wetu mpendwa, shukran
ReplyDelete