Mar 29, 2020

JE, MALKIA ELIZABETH WA UINGEREZA AMEAMBUKIZWA VIRUSI VYA CORONA

Baadhi ya duru zinadokeza kuwa Malkia Elizabeth ameambukizwa corona ingawa vyombo vya habari vya Uingereza vimenyamazia kimya taarifa hiyo.
Imedokezwa kuwa baada ya Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson kutangaza kuwa ameambukizwa corona mnamo Ijumaa, ripoti za kitibaz ilibaini kuwa Malikia Elizabeth pia ameambukizwa virusi hivyo.
Mwanamfalme Charles, aliye na umri wa miaka 71,  ambaye ni mrithi wa Ufalme wa Uingereza naye Jumatano alitangaza pia kuambukizwa corona na kusema atajiweka karantini katika kasri ya ufalme eneo la Scotland.
Mwanamfalme Charles ameambukizwa virusi vya corona
 Aidha Waziri wa Afya wa Uingereza Matt Hancock naye pia ameambukizwa corona.
Siku kadhaa zilizopita, vyombo vya habari vya Uingereza viliripoti kuwa, Malkia Elizabeth,93,  amelazimika kuhama kutoka kwenye kasri yake ya kifakhari iliyoko katikati ya London, mji mkuu wa Uingereza na kukimbilia katika maskani yake inayojulikana kwa jina maarufu la Windsor Castle kukwepa virusi vya corona.
Hadi kufikia Jumamosi watu 1,019 walikuwa wamefariki dunia kutokana na corona nchini Uingereza huku wengine zaidi ya 17,000 wakiwa wameambukizwa.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Pages