Monday, August 6, 2018

KANISA LA WAADVENTISTA WASABATO (SDA) LA KATA YA IYUMBU MKOANI SINGIDA LAPATA VYOMBO VYA MUZIKI KUPITIA HARAMBEE YA MBUNGE Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi, Mheshimiwa Elibariki Kingu (katikati), akisalimiana na waumini wa Kanisa la Waadventista Wasabato (SDA) la Kata ya Iyumbu wakati akiingia katika kanisa hilo kuendesha harambee ya changizo la kupata vyombo vya muziki vitakavyotumika kumtukuza mwenyezi mungu. Harambee hiyo ilifanyika jana katika kanisa hilo lililopo wilayani Ikungi mkoani humo ambapo jumla ya sh.milioni 4 zilipatika.
Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi, Mheshimiwa Elibariki Kingu, akizungumza na waumini hao wakati akianza kuendesha harambee hiyo.
 Waimbaji wa kwaya ya kanisa hilo wakiingia kwenye harambee kwa wimbo maalumu.
 Mbunge Kingu na waumini wa kanisa hilo wakiingia kanisani kwa ajili ya harambee.
 Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Kata ya Iyumbu (kulia), akiongoza kusali kabla ya kuanza kwa harambee hiyo.
 Kwaya ikitoa burudani.
 Waumini wakiwa kwenye harambee hiyo.
 Mzee wa Kanisa hilo, Marko Magadula akiongoza ibada kabla ya kuanza harambee hiyo.
 Wageni waalikwa wakiwa kwenye ibada hiyo. Kulia ni  Ahmed Hilal, mmiliki wa mabasi ya Sun set yanayofanya safari zake maeneo mbalimbali mkoani Singida,  ambaye katika harambee hiyo aliahidi kununu spika.
 Diwani wa Kata hiyo, Peter Gwiligwa akizungumza katika harambee hiyo.
 Katibu wa Mbunge, Abubakari Muna (kulia), akijumuika na waumini wa kanisa hilo katika harambee hiyo.
Waumini wa kanisa hilo wakiwa na watoto wao kwenye harambee hiyo.

Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

CCM Blog. Powered by Blogger.