Wednesday, July 4, 2018

SERIKALI YATOA MWEZI MMOJA BONYOKWA KULIMA MASHAMBA POLI


Na Heri Shaban
MANISPAA ya Ilala Dar es Salam imetoa mwezi mmoja mashamba poli yaliotekekezwa Mtaa wa Bonyokwa kuendelezwa.

Tamko hilo la mkurugenzi wa Manispaa Ilala lilitolewa na Ofisa MTENDAJI wa Kata ya Bonyokwa Josephat Sambua wakati wa kikao cha Wananchi Dar es salam jana.


Sembua alisema Mkurugenzi wa Manispaa ametoa maelekezo kuwataka wananchi wa Bonyokwa ambao wameyatelekeza mashamba poli kuyalima na kuanza hatua za ujenzi.

"Giografia ya Kata ya Bonyokwa ni makazi ya tambarale na milima  na sehemu nyingine mabonde, Bonyokwa imepakana na Segerea  ,Kisukuru na Kimanga.

Alisema changamoto kubwa ya Kata hiyo ambayo ina mitaa mitatu Bonyokwa, Bonyokwa Kisiwani na MTAA Msingwa wananchi wameshindwa kuyaendeleza hivyo ina hatarisha usalama wa wananchi.

Aliwataka wenye makazi yao kutumia fursa hii ambapo Mkurugenzi ametoa mwezi mmoja yawe yamelimwa na kuanza hatua za ujenzi.


Wakati huoho Ofisa MTENDAJI wa Bonyokwa Sambua alisema ameunda kamati ya Mpango shirishi wa Maendeleo ya shule.

Sambua alisema Mpango huo una lengo kuu la kutatua changamoto za shule zote za msingi  kwa kushirikiana na Wazazi na Walimu.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Mdau, andikamaoni yako hapa yasaidie kujua wewe unafikiri nini kuhusu posti hii. Tafdhali, Maoni yako yasiwe ya uchochezi wa aina yoyote.. Mawasiliano yetu:- simu +255 (0) 712 498008, Email: nkoromo@gmail.com.
Bashir Nkoromo
Msimamizi Mkuu, Blog ya Taifa ya CCM.

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

CCM Blog. Powered by Blogger.