Saturday, July 28, 2018

RAIS MAGUFULI AWATEUA VIJANA LUKUKI KUSHIKA NAFASI ZA UONGOZI: YUMO JERRY MURO, KAFULILA, KATAMBI, JOKATE NA WENGINE WENGI

IKULU, DAR ES SALAAM
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli, ameonyesha upendo na kuwajali vijana na kuondoa ule msemo uliozoeleka kuwa vijana ni taifa la kesho na badala yake sasa imekuwa vijana ni taifa la sasa, baada ya leo Jumamosi Julai 28, 2018 kuwateua vijana wengi katika nafasi mbalimbali za uongozi.

Rais pia ameonyesha imani kubwa kwa vijana kwa kumpandisha cheo Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam Ally Happy na sasa anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa.

Katika uteuzi huo ambao ulitangazwa moja kwa moja na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Rais DK Magufuli amemteua
Jerry Muro kuwa Mkuu mpya wa Wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha, 

Rais pia amemteua kijana mwingine Patrobas Katambi kuwa Mkuu mpya wa Wilaya ya Dodoma huku akimteua Moses Machali kuwa Mkuu mpya wa Wilaya ya Nanyumbu Mkoani Mtwara na Mwanamitindo na Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambaye amewahi kuwa katibu wa Hamasa na Chipikizi katika Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM),
Jokate Mwegelo akiteuliwa kuwa Mkuu mpya wa Wilaya ya Kisarawe Mkoani Pwani.

Ifuatayo ndiyo orodha kamili ya wateule wa Rais katika nafasi za Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya, Katibu Tawala wa Mkoa, Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu inapatikana hapo chiniShare:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

CCM Blog. Powered by Blogger.