LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 16, 2018

RAIS DKT. MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI CHUO CHA UONGOZI CHA MWALIMU JULIUS NYERERE KINACHOJENGWA KIBAHA KWA MFIPA MKOANI PWANI.

MWENYEKITI wa Chama cha Mapunduzi CCM na Rais Dkt John Magufuli amewataka wanachama wa Chama hicho kutembea kifua mbele nakudai kuwa kitaendelea kutawala kutokana na mikakati walioiweka katika chama hicho  na wanaohangaika na chama hicho watapata taabu Sana.


Rais Magufuli aliyasema hayo leo katika uwekaji jiwe la msingi katika ujenzi wa chuo cha uongozi cha Mwalimu Nyerere ambacho kinajengwa wilayani kibaha Kwa ushirikiano wa vyama sita rafiki wakiongozwa na Chama kimkomonisti cha china CPC.



Amesema chama hicho kitakuwepo na kitaendelea kuwepo hivyo wanaohangaika na chama hicho watapata tabu sana huku akiwataka makada wake kutembea kifua mbele kwa uimara uliojengwa na waasisi wa chama hicho.
Kuhusu ujenzi wa chuo



Akizungumzia ujenzi wa chuo hicho mbele ya Waziri wa Mambo ya nje kutoka chama cha CPC. Song Tao .Dkt Magufuli amesema  kwanza anawapongeza viongozi wastaafu Rais wa awamu ya nne  Dkt Jakaya Kikwete, Makamu Mwenyekiti Philipo Mangula, pamoja na Katibu mkuu mstaafu. Komred Abdulrahman Kinana.



Amesema viongozi hao kwa pamoja walifanya kazi kubwa kuendesha mazungumza na nchi vyama rafika na kufikia muafaka wa kujenga chuo hicho leo ambapo yeye anamalizia kazi ambayo wao wameshaifanya.



"Nataka niseme nawapongeza mno wazee hawa ambao wamefanya kazi kubwa ya kufikia makubaliano ya kujenga chuo hiki hapa Pwani moja ya mkoa ambao ulishiriki kupambania ukombozi ambapo kambi yake iliwekwa Kaole Bagamoyo. "alisema Magufuli



Nakuongeza kuwa chuo hicho matarajio yake watapikwa wanasiasa ili kutoa viongozi waliopikwa Kwa uweledi kwa maendeleo ya nchi hizo sita za afrika zinazounganishwa na chama cha Cpc pamoja na Chama cha Mapinduzi Kwa upande wa Afrika. "alisema



Magufuli alisema mbali na makada kutoka katika nchi hizo rafiki lakini hawatakuwa na ubaguzi kwani chuo hicho kitakuwa ndio dira ya kweli ya kuleta ukombozi wa kweli wa kiuchumi.



"wakati ule tulipambana kwa ajili ya kupigania ukombozi wetu natuliupata hivyo chuo hiki sasa pamoja na mambo mengine kitapigia ukombozi wa kukuwa kwa uchumi wetu"alisisitiza Magufuli



  Dkt Magufuli pia alitumia fursa hiyo kuwashukuru nchi zote sita kukubali kwamba chuo hicho kijengwe Tanzania huku wakitambua mchango mkubwa wa taifa kupitia kazi kubwa aliyoifanya Hayati Mwalimu Nyerere ya kupigania ukombozi wa nchi za afrika pamoja na waasisi wengine wa nchi za afrika.



                Kuhusu Masomo



Pia Rais Magufuli akizungumzia namna ya uendeshaji wa chuo hicho aliwataka makatibu wakuu wa vyama hivyo rafiki yaani FRELIMO,  MPLA, ZANU-PF SWAP na ANC kuharakisha mchakato wa kutengeneza mtaala wa kufundishia huku akiwataka wasijikite kufundisha itikadi tu badala yake aafundishe na masomo ya kuleta mageuzi ya kiuchumi.



"Nawaomba mkae haraka ili kupanga mtakavyo endesha chuo hiki maana nataka kikamilika na nyie mnaaza mara moja kufundisha na mfundishe hadi masomo ya Development Study. "Alisema Magufuli



Aidha Rais Magufuli aliwataka viongozi hao kuwakaribisha na watu kutoka vyama vingine hususani vyenye mtazamo kama wao ili nao wapikwe na wawe viongozi bora katika nchi zao.



        Mkandalasi



Rais Magufuli alimtaka mkandalasi anayejenga chuo hicho ambao ni kampuni ya RJM kuharakisha ujenzi wa chuo hicho kwani hakuna sababu ya kuchelewa wakati fedha zipo.



"Nawaomba kukamilisha ujenzi huu  wa chuo hiki haraka na Naomba muwatumie wananchi wa kibaha ili kushiriki kikamilifu katika ujenzi huu nakudai vijana kuchangamkia ajira hiyo. "Alisema Magufuli



Nakuongeza kuwa kukamilika kwa chuo hicho kitatoa mchango mkubwa kwa ajili ya kuleta uchumi huku akiwataka wananchi hao kuepuka kuiba vifaa vya ujenzi huo



Aidha Magufuli alimtaka mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndekilo kuhakikisha wanatengeneza barabara ya kuelekea chuoni hapo kwa kushirikiana na wakala wa barabara Tanroad  kwani chuo hicho ni cha kimataifa lazima kiwe na barabara nzuri.



          Gharama za ujenzi



Rais Magufuli alisema katika kukamilisha ujenzi wa chuo hicho tayari dola milioni arobaini na tano (45) sawa na shilingi bilioni 100 za kitanzania zimetengwa na fedha hizo ni msaada kutoka kwa rais wa china  Xi Jinping .



Alisema nchi ya china ni rafiki wakweli na misaada yao hawakuaza kutoa miaka bali tangu enzi hizo kwani walishatoa hadi silaha kwa ajili ya kusaidia Tanzania ikiwa pamoja na misaada mingine kama ujenzi wa reli ya Tazara.



"Nakuomba mh.waziri nenda kanipelekee salamu zangu kwa rais wa china na sisi kama Tanzania tutaendelea kushirikiana nae."alisema



Kwa upande wake waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa kimataifa kutoka chama CPC . song Tao Akisoma barua ya rais wa china alisema rais huyo kapongeza tukio hilo ambalo msingi wake  ni kuendeleza mshakamano uliopo



Alisema rais wa china amezihakikishia nchi hizo sita za hususani zenye urafiki na CPC kuwa vyama hivyo vitaendelea kuimarisha  na kushauriana  ikiwa pamoja na kubadilisba uzoefu.



Alisema rais wa china anatoa baraka zake kwa ujenzi wa chuo hicho   ambapo malengo na matumaini yao  kuendeleza undugu  ili  kuyafikia maendeleo.



Kwa upande wa makatibu hao ambao wote walipata nafasi ya kuzungumza mbele ya rais walisema wanaitambua Tanzania kwa mchango mkubwa walioutoa katika harakati za kupigania ukombozi



Walisema Tanzania kupitia Mwalimu Nyerere sambamba na viongozi wengine waasisi wa afrika walifanya kazi kubwa kuhakikisha wanapata ukombozi na kwamba kupitia chuo hicho ni matumaini yao kitapika viongozi wengine wenye uzalendo kama Mwalimu Nyerere.



Makatibu  wa vyana waliohudhuria ni pamoja na Dkt Bashir All CCM, Antonio Kasoma Angola, Obart Pof, Zimbabwe, RoQei Silva Msumbiji, Sophia shanagwa Namibia,  na Ace Magashure. Ambapo wote kwa pamoja wanashiriki mkutano wa Dunia kwa siku mbili ambapo Mwenyeji wake ni Rais Dkt  John Magufuli ambaye ni Mwenyekiti wa CCM .

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Waziri wa uhusiano wa Kimataifa wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Song Tao wanne kutoka kushoto pamoja na Makatibu wa vyama vya, CCM, ANC, SWAPO, ZANU-PF, MPLA, FRELIMO, wakiweka mchanga kama ishara ya uwekaji wa Jiwe la msingi Ujenzi wa Chuo cha Mwalimu Julius Nyerere kinachojengwa katika eneo la Kibaha kwa mfipa mkoani Pwani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Waziri wa uhusiano wa Kimataifa wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Song Tao wanne kutoka kushoto pamoja na Makatibu wa vyama vya, CCM, ANC, SWAPO, ZANU-PF, MPLA, FRELIMO, wakiweka mchanga kama ishara ya uwekaji wa Jiwe la msingi Ujenzi wa Chuo cha Mwalimu Julius Nyerere kinachojengwa katika eneo la Kibaha kwa mfipa mkoani Pwani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na mgeni wake Waziri wa uhusiano wa Kimataifa wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Song Tao wanne kutoka kushoto waliokaa, viongozi wa vyama vya ANC, SWAPO,ZANU-PF, MPLA, FRELIMO pamoja na viongozi mbalimbali wa Chama cha Mapinduzi CCM mara baada ya kuweka jiwe la msingi ujenzi wa Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Julius Nyerere kinachojengwa katika eneo la Kibaha kwa mfipa mkoani Pwani. Chuo hicho kinajengwa na Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) kwa gharama ya Shilingi Bilioni mia moja(100). 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na mgeni wake Waziri wa uhusiano wa Kimataifa wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Song Tao kabla ya tukio la uwekaji jiwe la msingi ujenzi wa Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Julius Nyerere kinachojengwa katika eneo la Kibaha kwa mfipa mkoani Pwani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli akipiga ngoma pamoja Sophia Shaningwa Katibu wa Chama cha SWAPO kutoka nchini Namibia huku Waziri wa uhusiano wa Kimataifa wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Song Tao akipiga makofi mara baada ya uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi wa Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Julius Nyerere kinachojengwa katika eneo la Kibaha kwa mfipa mkoani Pwani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli akipiga ngoma na Katibu wa Chama cha SWAPO kutoka Namibia Sophia Shaningwa pamoja na Waziri wa uhusiano wa Kimataifa wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Song Tao mara baada ya kuweka jiwe la msingi ujenzi wa Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Julius Nyerere kinachojengwa katika eneo la Kibaha kwa mfipa mkoani Pwani. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli akipiga ngoma na Waziri wa uhusiano wa Kimataifa wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Song Tao mara baada ya kuweka jiwe la msingi ujenzi wa Chuo cha Mwalimu Julius Nyerere kinachojengwa katika eneo la Kibaha kwa mfipa mkoani Pwani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi kabla ya ya kuweka jiwe la msingi ujenzi wa Chuo cha Uongozi cha Uongozi cha Mwalimu Julius Nyerere kinachojengwa katika eneo la Kibaha kwa mfipa mkoani Pwani. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia mfano wa moja ya majengo ya chuo hicho kitakapo kamilika kujengwa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli akipunga mkono kwa wananchi(hawaonekani pichani) wakati akiwasili katika eneo kitakapojengwa Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Julius Nyerere Kibaha kwa mfipa mkoani Pwani. (PICHA NA IKULU)

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages