LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 4, 2018

NAIBU WAZIRI OLE NASHA ATEMBELEA BANDA LA VETA SABA SABA



NAIBU Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha amesema asilimia 66 ya wanafunzi wanaomaliza katika Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) wanaweza kujiajiri wenyewe.

Aidha amesema Serikali itaendelea kutilia mkazo kwenye elimu ya ufundi stadi kwani ni muhimu katika kukuza uchumi wa viwanda nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam  mara baada kutembelea baadhi ya mabanda yaliyopo katika Maonyesho ya 42 ya kimataifa ya Biashara yaliyopo Viwanja vya Sabasaba, Ole Nasha alisema wanajivunia VETA kwa sababu wamekuwa wakitoa wataalam mbalimbali wanaoweza kujiajiri.


Amesema kuwa anatambua kuwa nchi haiwezi kuwa na viwanda kama haitakuwa na wataalam wa kutosha wenyewe ujuzi hivyo wataendelea kuweka msisitizo katika hilo na kuboresha mazingira ya wanafunzi na ufundishaji katika vyuo vya ufundi stadi.


"Huwezi kuwa na viwanda kama una mafundi wa kutosha, sasa hivi kwa mwaka katika vyuo vyetu vya serikali vya ufundi stadi uzalisha wanafunzi 150,000 ambao umaliza masomo yao na kujiajiri na wengine kuajiliwa," amesema  Ole Nasha.

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages