LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 5, 2018

UKAGUZI WA MAGARI KILIMANJARO WABAINI , MADEREVA KUTUMIA LESENI ZA NDUGU ZAO


Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,ACP.Hamis Issah akitoa maelekezo kwa Mkuu wa Operesheni wa kikosi cha Usalama Barabarani,Mkaguzi ,Peter Mizambwa wakati wa ukaguzi huo uliofanyika katika kituo kikuu cha Mabasi mjini Moshi.
Mkuu wa Operesheni wa Kikosi cha Usalama barabarani mkoa wa Kilimanjaro,Inp Peter Mizambwa  akimuonesha kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,ACP,Hamis Issah moja ya karatasi ambazo zinatumiwa na madereva kama Leseni.
Mkuu wa Operesheni wa Kikosi cha Usalama barabarani mkoa wa Kilimanjaro,Inp Peter Mizambwa  akimuonesha kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,ACP,Hamis Issah alama za leseni ambayo ni halisi .
Kamanda Issah akitoa maelekezo kwa askari wake.
Mmoja wa Madereva waliokaguliwa akionesha vipande vya karatasi ambavyo alidai kuwa ni leseni .
Mkaguzi wa Magari akikagua  moja ya mabasi yaliyokuwa yafanye safari ya kuelekea Dar es Salaam .
Kamanda wa Polisi akimuuliza mmoja wa madereva  waliokamatwa ,matumizi ya silaha ya Kisu kilichokutwa katika gari lake.
Mmoja wa Madereva akipelekwa kituo cha Polisi mara baada ay kubainika kutumia leseni ya ndugu yake kuendesha gari.

Na Dixon Busagaga  wa Globu ya Jamii KAnda ya Kaskazini.

UKAGUZI wa Magari ya Abiria pamoja na Leseni unaofanywa na Jeshi la Polisi mkoa  wa Kilimanjaro umebaini udanganyifu mkubwa unaofanywa na baadhi ya Madereva wa Magari ya abiria ukiwemo kuendesha bila  Leseni ,Umri  wa kuendesha gari kupitiliza , wengine wakitumia Leseni za Ndugu zao.

Katika kituo Kikuu cha Mabasi ya abiria yaendayo mikoani na yale yanayofanya safari zake ndani ya mkoa wa Kilimanjaro,Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro Hamisi Issah akiwa ameongozana na Mkuu  Operesheni kikosi cha usalama Barabarani ,Peter Mizambwa na maofisa wengine wa Polisi wamefanya ukaguzi.

Katika ukaguzi huo magari zaidi ya 800 yamekaguliwa na yaliyobainika kuwa mabovu yalizuiliwa kuendelea na safari huku  baadhi ya Madereva wakikutwa  na silaha katika magari yao vikiwemo Visu,kamanda Issah akatoa onyo kwa madereva kutembea na silaha pamoja na kujaza abiria hali inayochangia abiria kukaa katika mikao isiyo rafiki .

Mkuu wa operesheni wa kikosi cha usalama barabarani ,Mkaguzi wa Polisi Peter Mizambwa akazungumzia Operesheni Nyakua iliyoanza kwa lengo la kupunguza ajali  huku baadhi ya Madereva na wananchi wakipongeza utaratibu huo.

Mwisho.
KAWAIDA . Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,ACP,Hamis Issah akitembelea kikuu cha Mabasi mjinib Moshi kwa ajili ya ukaguzi wa Magari ya Abiria. Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,ACP.Hamis Issah akitoa maelekezo kwa Mkuu wa Operesheni wa kikosi cha Usalama Barabarani,Mkaguzi ,Peter Mizambwa wakati wa ukaguzi huo uliofanyika katika kituo kikuu cha Mabasi mjini Moshi. Mkuu wa Operesheni wa Kikosi cha Usalama barabarani mkoa wa Kilimanjaro,Inp Peter Mizambwa akimuonesha kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,ACP,Hamis Issah moja ya karatasi ambazo zinatumiwa na madereva kama Leseni. Mkuu wa Operesheni wa Kikosi cha Usalama barabarani mkoa wa Kilimanjaro,Inp Peter Mizambwa akimuonesha kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,ACP,Hamis Issah alama za leseni ambayo ni halisi . Kamanda Issah akitoa maelekezo kwa askari wake. Mmoja wa Madereva waliokaguliwa akionesha vipande vya karatasi ambavyo alidai kuwa ni leseni . Mkaguzi wa Magari akikagua moja ya mabasi yaliyokuwa yafanye safari ya kuelekea Dar es Salaam . Kamanda wa Polisi akimuuliza mmoja wa madereva waliokamatwa ,matumizi ya silaha ya Kisu kilichokutwa katika gari lake. Mmoja wa Madereva akipelekwa kituo cha Polisi mara baada ay kubainika kutumia leseni ya ndugu yake kuendesha gari. Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii KAnda ya Kaskazini. UKAGUZI wa Magari ya Abiria pamoja na Leseni unaofanywa na Jeshi la Polisi mkoa wa Kilimanjaro umebaini udanganyifu mkubwa unaofanywa na baadhi ya Madereva wa Magari ya abiria ukiwemo kuendesha bila Leseni ,Umri wa kuendesha gari kupitiliza , wengine wakitumia Leseni za Ndugu zao. Katika kituo Kikuu cha Mabasi ya abiria yaendayo mikoani na yale yanayofanya safari zake ndani ya mkoa wa Kilimanjaro,Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro Hamisi Issah akiwa ameongozana na Mkuu Operesheni kikosi cha usalama Barabarani ,Peter Mizambwa na maofisa wengine wa Polisi wamefanya ukaguzi. Katika ukaguzi huo magari zaidi ya 800 yamekaguliwa na yaliyobainika kuwa mabovu yalizuiliwa kuendelea na safari huku baadhi ya Madereva wakikutwa na silaha katika magari yao vikiwemo Visu,kamanda Issah akatoa onyo kwa madereva kutembea na silaha pamoja na kujaza abiria hali inayochangia abiria kukaa katika mikao isiyo rafiki . Mkuu wa operesheni wa kikosi cha usalama barabarani ,Mkaguzi wa Polisi Peter Mizambwa akazungumzia Operesheni Nyakua iliyoanza kwa lengo la kupunguza ajali huku baadhi ya Madereva na wananchi wakipongeza utaratibu huo.

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages