Sunday, July 16, 2017

WAZIRI MKUU AENDA KUTOA POLE NYUMBANI KWA DK. MWAKYEMBE, RAIS JPM ATUMA SALAM ZA RAMBIRAMBI


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisaini kitabu cha maombolezo,alipo hudhuria msibani kwa aliyekua Mke wa Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe, Linah Mwakyembe, aliyefariki katika Hospitali ya Agakhan leo alfajiri. Julai 16, 2017. 
Mke wa Waziri Mkuu Kassim Mary Majaliwa, akisaini kitabu cha maombolezo,alipo hudhuria msibani kwa aliyekua Mke wa Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe, Linah Mwakyembe, aliyefariki katika Hospitali ya Agakhan leo alfajiri. Julai 16, 2017. 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,akizungumza na Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe, alipo hudhuria msibani kwa aliyekua Mke wa Dr. Harrison Mwakyembe, Linah Mwakyembe, aliyefariki katika Hospitali ya Agakhan leo alfajiri. Julai 16, 2017. 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akimkabidhi mchango wa rambirambi Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe,alipo hudhuria msibani kwa aliyekua Mke wa Dr. Harrison Mwakyembe, Linah Mwakyembe, aliyefariki katika Hospitali ya Agakhan leo alfajiri. Julai 16, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
-------------------------------------------------------------------

RAIS DK. MAGUFULI ATUMA SALAM ZA RAMBIRAMBI
Rais Dk. John Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harrison George Mwakyembe kufuatia kifo cha mkewe Linah George Mwakyembe kilichotokea usiku wa tarehe 15 Julai, 2017.

Linah George Mwakyembe amefariki dunia katika hospitali ya Agha Khan Jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.

Taarifa iliyotolewa na Ikulu jjini Dar es Salaam, leo imesema, katika salamu hizo, Rais Magufuli ameelezea kushtushwa na kusikitishwa na kifo hicho, na amesema yeye na familia yake wanaungana na familia ya Dk. Mwakyembe katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.

“Nakupa pole sana Dk. Mwakyembe kwa kuondokewa na mkeo mpendwa Bi. Linah, natambua hisia za maumivu ulizonazo wewe na familia nzima, nyote nawaombea Mwenyezi Mungu awatie nguvu, awape subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.

Namuombea Marehemu Linah George Mwakyembe apumzishwe mahali pema peponi, Amina” Taarifa hiyo imemkariri Rais Magufuli akisema.
Share:

KUCHAGUA LUGHA

IDADI YA WATU AMBAO HUTEMBELEA BLOGU HII

KUMBUKUMBU ZA POSTI ZOTE

JISAJILI UPATE TAARIFA KWA EMAIL

Jisajili ili upate taarifa kwa email

Google+ Followers

Powered by Blogger.