Saturday, June 3, 2017

RAIS DK. MAGUFULI ATEUA MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO NA MABALOZI WAWILI, LEO

Ikulu, Dar es Salaam.
Rais Dk. John Pombe Magufuli leo Juni 3, 2017 amemteua Anna Elisha Mghwira kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, kuchukua nafasi iliyoachwa na Said Meck Sadiki aliyejiuzulu hivi karibuni.

Wakati huo huo, Rais Magufuli amemteua Meja Jenerali Issah Suleiman Nassor kuwa Balozi ambaye kabla ya uteuzi huo alikuwa Mkuu wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ).

Pia Rais Magufuli amemteua DIGP Abdulrahman Omari Juma Kaniki kuwa Balozi ambaye alikuwa Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi. Taarifa ya Ikulu imesena tarehe ya kuapishwa kwa wateule wote itatangazwa baadaye

Share:

KUCHAGUA LUGHA

IDADI YA WATU AMBAO HUTEMBELEA BLOGU HII

KUMBUKUMBU ZA POSTI ZOTE

JISAJILI UPATE TAARIFA KWA EMAIL

Jisajili ili upate taarifa kwa email

Google+ Followers

Powered by Blogger.