KINANA: FOMU ZA KUWANIA UONGOZI CCM HAZIUZWI, WALIOUZIWA WADAI KUREJESHEWA FEDHA ZAO

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Abdulrahman Kinana amesema ni marufuku kuuzwa fomu za uchaguzi kwa ngazi zote za uongozi ndani ya Chama kwa mgombea na kuagiza mwanachama yeyote aliyeuziwa fomu adai kurejeshewa fedha zake.

Taarifa iliyosainiwa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rodrick Mpogolo kwenda kwa Makatibu Wakuu wa Jumuiya imesema.