Tuesday, May 2, 2017

WAZEE WA CCM Z'BAR WATOA WAMPONGEZA DR.SHEIN NA KUTOA MAPENDEKEZO MAZITO

Na Mwandishi Wetu
Baraza la Wazee wa Chama Cha Mapinduzi ((CCM) Zanzibar kwa niaba ya wazee wote wa Chama hicho linampongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Ali Mohammed Shein kwa kutimiza ahadi yake ya kuinua kiwango cha chini cha Mishahara kwa asilimia 100 kwa watumishi wa Umma, hatua iliyoanzia mwezi wa April, 2017.

Pia wamemuomba Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kuendelea kusimamia kwa umakini mambo matatu; Kuwabana wasiolipakodi hasa baadhi ya wafanyabiashara wenye tabia za ukwepaji wa kodi hizo,  Kusimamia Bodi zinazoshughulikia masuala ya upandaji wa bei za bidhaa ili kuzuwia mfumko wa bei hizo zinazopanda bila ya kuzingatia kipato cha wananchi na afanye tathmini zitakazosaidia kusimamia rasli mali za Zanzibar ili zitumike kwa uangalifu zaidi kwa kuwanufaisha wananchi wote.

"Aidha, tumefurahishwa na tukio la kupunguza kodi ya mapato kutoka kiwango cha asilimia 13% hadi asilimia 9% Lakini pia kusimamia na kuwajibisha watendaji wasio waaminifu kwa Serikali,.

Pamoja na pongezi zetu wazee tunatoa nasaha kwa watumishi wa Umma kwa kuwaomba wafanye kazi kwa bidii na uadilifu. Mwisho sisi wazee tunawatakia mema wafanyakazi wa SMZ katika maisha yao na tunamuombea Mhe. Rais Dk. Ali Mohamed Shein na familia yake maisha mema, afya bora na mafanikio makubwa" Imesema taarifa ya baraza hilo la wazee.

Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.