RAIS DK. MAGUFULI AREJEA DAR LEO BAADA YA ZIARA YA MKOA WA KILIMANJARO

Moshi, Kilimanjaro
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli, leo tarehe 02 Mei 2017, amemaliza ziara ya siku tatu mkoani Kilimanjaro, ambapo akiwa mkoani humo pamoja na mambo mengine alikuwa mgeni rasmi katika Maadhimisho ya siku ya Wafanyakazi Duniani - Mei Mosi.

Taarifa iliyotolewa na Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Jaffar Haniu, imesema, katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Kilimanjaro - KIA, Rais Magufuli ameagwa na viongozi mbalimbali wa mkoa huo wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Said Mecky Saidicky na na Mkuu wa Wilaya ya Hai Gelasius Byakanwa.

Raais Dk John Magufuli akiwaaga wananchi baada ya kupata Ndege kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) tayari kujerea Dar es Salaam, leo

0 comments:

Post a Comment

Mdau, Uwanja huu ni wako, Toa maoni yako yasaidie kujua wewe unafikiri nini kifanyike kuboresha zaidi maisha ya Watanzania. Maoni yako yasilenge kuchochea mtafaruku katika jamii, kisiasa, kidini, kikabila au kijinsia. Mawasiliano yetu:- simu +255 (0) 712 498008, Email: nkoromo@gmail.com.
Bashir Nkoromo
Msimamizi Mkuu, Blog ya Taifa ya CCM.