LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

May 23, 2017

RAIS DK ,MAGUFULI AMTEUA NDUGURU KUWA NAIBU MKURUGENZI MPYA TRA

Ikulu, Dar es Salaam
Rais Dk. John Magufuli amemteua Adolf Hyasinth Mohondela Ndunguru kuwa Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Adolf Hyasinth Mohondela Ndunguru ambaye kabla ya uteuzi huo alikuwa Kamishna wa Sera, Wizara ya Fedha na Mipango, anachukua nafasi iliyoachwa na Charles Edward Kichere ambaye hivi karibuni aliteuliwa kuwa Kamishna Mkuu wa TRA.

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa imesema, uteuzi wa Adolf Hyasinth Mohondela Ndunguru umeanza jana, Mei 22, 2017.

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages