LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

May 10, 2017

NGEMELA AWATAKA VIONGOZI NA WANACHAMA WA CCM KUWAELIMISHA WANANCHI WASIOIJUA VEMA CCM

DODOMA.
Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga, amesema wanachama na viongozi wa CCM wanaikielewa vema Chama, wanapaswa kuwaelimisha wananchi wote ili kuwa na uelewa wa pamoja, kuhusu lengo na misingi ya Chama.

Lubinga amesema hayo, jana wakati akifungua semina elekezi kwa Makatibu Kata wa CCM, Kata zote za wilaya ya Dodoma mjini iliyokuwa na lengo la kuwajengea uwezo na kuwaweka tayari kwa uchaguzi wa chama kuanzia ngazi hiyo ya kata, iliyofanyika katika Ukumbi wa NEC, makao Makuu ya CCM mjini Dodoma.

Amesema, ni vema kufanya hivyo kwa kuwa inawezekana bado wapo wananchi ambao hawaekielewi vizuri Chama Cha Mapinduzi kwa sababu ya kutokuwa na elimu ya kutosha, kwani hata mafanikio yaliyopatikana kutokana na uchaguzi uliopita kwa wilaya ya Dodoma mjini kufanya vizuri, siyo wana CCM tu walikipigia kura Chama.

“Hayati Mwalimu Nyerere alipolala akaota kuhamishia Makao Makuu ya nchi mkoani Dodoma alijua kuwa ninyi mnajua nchi hii inataka na inafanya nini, kwa sababu hivi vitu haviji hivihivi tu hata wazee wetu hawa wa zamani wanaelewa kuwa hakuna mtu aliyemshawishi Mwalimu Nyerere ahamishie makao makuu hapa” Alisema Lubinga.

Ngemela aliwataka viongozi na wanachama hao kuondokana na mazoea ya zamani ambayo waliyazoea kwani kwa sasa chama kinayafanya marekebisho makubwa kimfumo na hali hiyo inaweza kuleta kutoeleweka kwa baadhi ya wanachama.

Amewataka viongozi waliopewa dhamana kuacha kulialia bali wawajibike kama Baba au Mama anavyowajibika katika familia na kuonya kuwa viongozi wanaofanya kazi kwa mazoea na kutofanya majukumu yao watachukulia hatua kutokana na kutafuata utaratibu katika nafasi zao.

Mapema, Lubinga aliwataka washiriki wa semina hiyo kusimama kwa dakika mbili ili kuomboleza vifi vya wanafunzi 32, walimu wawili na dereva,  waliofariki katika ajali ya basi mkoani arusha May 6, 2017.

Akisoma taarifa ya uchaguzi katibu wa CCM wilaya ya Dodoma mjini Pili Augustino, alisema Uchaguzi unaendelea katika mashina na kata ambazo hazijafanya uchaguzi huku akiwataka wanachama kuchangamkia fomu.

“Chama kinaendelea kusimamia jumuia zake ili ziweze kufanya uchaguzi ili kuendana na ratiba iliyopangwa, pia madarasa, makambi ya wanachama yarejeshwe kwa ngazi zote ili kuwafundisha wanachama wetu katika misingi ya uwajibikaji na uzalendo”. alisema Katibu huyo.
Katibu wa CCM wilaya ya Dodoma mjiji Pili Augustino akizungumza wakati wa semina hiyo

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages