LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 7, 2017

RAIS AMTUMBUA MTENDAJI MKUU SHIRIKA LA ELIMU KIBAHA

Rais wa John Magufuli ametengua  uteuzi wa Mtendaji  Mkuu wa Shirika  Elimu Kibaha  Dk. Crispin  Mpemba  ili kupisha uchunguzi wa tuhuma mbalimbali za kiutendaji zinazomkabili.

Akijibu swali la Waandishi wa Habari waliotaka kupata ufafanuzi juu ya hatma ya tuhuma mbalimbali zinazolikabili Shirika la Elimu Kibaha ambazo zimekuwa zikiandikwa kwenye vyombo vya habari kwa muda mrefu sasa, Simbachawene alisema kutokana na kuwepo kwa tuhuma mbalimbali za uendeshaji, Rais  Magufuli tarehe  4/3/2017  ametengua rasmi nafasi ya Mtendaji huyo ili kupisha uchunguzi.

“ Ni kweli tuhuma juu ya uendeshaji wa Shirika la Elimu Kibaha likiwemo suala la Mikataba iliyoingiwa na Shirika hilo zimekuwepo kwa muda mrefu sasa. Sisi kama Wizara hatukutaka kukurupuka kufanya maamuzi na tukaamua kuunda kikosi kazi ili kufanya uchunguzi na matokeo ya uchunguzi huo  yanapelekea kuwepo kwa hoja  zinazohitaji uchunguzi zaidi.

Hivyo, ili uchunguzi huo uweze kufanyika  Mhe. Rais amemsimamisha kazi Mtendaji huyu Mkuu wa Shirika la Elimu Kibaha ili kupisha uchunguzi wa kina dhidi yake", alisema Simbachawene.

Alisema uamuzi wa kumsimamisha umechukuliwa kwakuwa tuhuma za awali zilizojitokeza dhidi yake zinajenga hoja ya kuhitajika kufanyika kwa uchunguzi zaidi. Kwa sasa nafasi ya Mtendaji Mkuu wa Shirika la Elimu Kibaha inakaimiwa hadi hapo  uchunguzi utakapokamilika.

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages