MPOGOLO ASHAURI HALMASHAURI KUALIKA TAASISI NA MASHIRIKA MATIKA MAZOEZI

Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam, Edward Mpogolo ameiomba Halmashauri kupitia Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kuangalia uwezekano wa kuzialika taasisi na mashirika mbalimbali katika mazoezi wanayokuwa wanafanya kila Jumamosi ya pili ya kila mwezi kama ilivyoagizwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu, na yale ya kila Ijumaa kama walivyojipangia wao.

DAS Mpogolo ameyasema hayo jijini Dar es Salaam katika viwanja vya Jakaya M. Kikwete Youth Park nakufafanua kuwa kufanya hivyo kunaongeza mahusihano mema kati ya watumishi wa serikali na mashirika au taasisi binafsi na hatimaye kuweza kusaidiana kwa baadhi ya masuala yenye tija kwa jamii.0 comments:

Post a Comment

Mdau, Uwanja huu ni wako, Toa maoni yako yasaidie kujua wewe unafikiri nini kifanyike kuboresha zaidi maisha ya Watanzania. Maoni yako yasilenge kuchochea mtafaruku katika jamii, kisiasa, kidini, kikabila au kijinsia. Mawasiliano yetu:- simu +255 (0) 712 498008, Email: nkoromo@gmail.com.
Bashir Nkoromo
Msimamizi Mkuu, Blog ya Taifa ya CCM.