KIKAO CHA BARAZA KUU MAALUM UVCCM TAIFA, KUFANYIKA MACHI 09, MJINI DODOMA

Na FAHADI SIRAJI
Umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) , umepanga kufanya kikao cha Baraza kuu  Maalum , Machi 09, 2017  kitakacho tanguliwa na kikao cha kamati ya Utekelezaji ya Baraza kuu  UVCCM Taifa mjini Dodoma .
Taarifa iliyosainiwa na Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka,imesema kikao hicho Maalum kinafanyika kwa ajili ya kupokea mapendekezo ya marekebisho ya kanuni ya Umoja wa Vijana wa CCM kufuatia maboresho yanayo tarajiwa kufanyika katika katiba ya Chama Cha Mapinduzi Toleo la 1977 marekebisho ya 2017.
Aidha Baraza kuu Maalum Litafanya mabadiliko ya Miongozo na taratibu za Umoja wa Vijana CCM.

Mabadiliko na Maboresho ya kanuni na Miongozo hiyo ni kuendana na matakwa ya katiba ya Chama Cha Mapinduzi.

 Ifuatayo ni Taarifa rasmi, tafadhali isome upate taarifa kwa kina...


0 comments:

Post a Comment

Mdau, Uwanja huu ni wako, Toa maoni yako yasaidie kujua wewe unafikiri nini kifanyike kuboresha zaidi maisha ya Watanzania. Maoni yako yasilenge kuchochea mtafaruku katika jamii, kisiasa, kidini, kikabila au kijinsia. Mawasiliano yetu:- simu +255 (0) 712 498008, Email: nkoromo@gmail.com.
Bashir Nkoromo
Msimamizi Mkuu, Blog ya Taifa ya CCM.