TAKWIMU ZADAI WATANZANIA BADO WANAKABILIWA NA TATIZO LA UDUMAVU WA AKILI NA MWILI

Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC) Dk. Joyce Kaganda akizungumza katika Mkutano wa wa siku tatu wa uhamasishaji wa Afya na lishe kwa vijana (hasa kwa wasichana), ulioanza leo katika kumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.

Dar es Salaam
Takwimu ya hali ya lishe nchini kwa mwaka 2015/16 inaonyesha kuwa bado kuna uwepo wa hali ya tatizo la udumavu kwa watanzania hususani katika udumavu wa akili na mwili.

Akizungumza hayo Dar es Salaam jana,Mkurugenzi Msaidizi wa Lishe wa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt Vicent Assey wakati wa mkutano wa wadau mbalimbali wa Afya nchini, alisema sababu kubwa ya watoto kuzaliwa na hali ya udumavu ni kutokuwepo na mpangilio mzuri wa vyakula.

Alisema jamii bado inachangamoto ya kutojua lishe bora kwa wakati muafaka inayozingatia mlo kamili na kujua ni wakati gani chakula kinatakiwa kuliwa kwa mtoto.

Dkt Assey alisema serikali inaendelea kuweka nguvu katika kusaidia kutatua tatizo hilo ambapo hadi sasa tatizo hilo limepungua kutoka asilimia 42 hadi 34.

Alisema kutokana na takwimu hizo inaonyesha hali imeanza kuwa nzuri kwa kutatua  tatizo hilo ambapo kuna baadhi ya mikoa iliyofanya vizuri katika kutokomeza hali hiyo ikiwemo Dar es Salaam ikionyesha hali ya udumavu ni asilimia 14.6 huku mikoa mingine bado hali yake sio nzuri katika tatizo hilo.

Kwa Upande wake Mkurugenzi Mkazi wa taasisi ya Micro  nutrient inifiative,Dkt Daniel Nyagawa alisema mkutano huo umejumuisha wadau mbalimbali kutoka serikalini,mashirika ya kimataifa, taasisi zisizokuwa za kiserikali kutoka katika nchi nne ikiwemo Senegal,Ethiopia,Kenya na Tanzania.

0 comments:

Post a Comment

Mdau, Uwanja huu ni wako, Toa maoni yako yasaidie kujua wewe unafikiri nini kifanyike kuboresha zaidi maisha ya Watanzania. Maoni yako yasilenge kuchochea mtafaruku katika jamii, kisiasa, kidini, kikabila au kijinsia. Mawasiliano yetu:- simu +255 (0) 712 498008, Email: nkoromo@gmail.com.
Bashir Nkoromo
Msimamizi Mkuu, Blog ya Taifa ya CCM.