LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jan 2, 2017

RAIS DK. MAGUFULI AWATAKA WAKUU WA WILAYA NA MIKOA KUONDOA UTITIRI WA KODI KATIKA MAZAO

Na Daudi Manongi - MAELEZO
Rais Dk. John amewataka Wakuu wa Mikoa, Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri kuondoa utitiri wa kodi uliopo kwenye mazao ili wakulima waweze kunufaika kutokana na kujiongezea kipato.

Rais Magufuli ametoa agizo hilo leo wakati akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uiofanyika Wilaya ya Bukoba, akiwa katika ziara yake ya kikazi ya siku mbili aliyoainza jana mkoani Kagera.

“Nawaagiza Wakuu wa Mikoa, Wilaya pamoja na Wakurugenzi wa Halmashauri kupitia upya kodi zilizopo katika bidhaa mbalimbali kama Kahawa na Pamba, hakikisheni mnaondoa utitiri huu wa Kodi ili wafanyabiashara hawa wafaidike na mazao yao,” Alisema Rais Magufuli.

Aidha Rais Magufuli amewaahidi watanzania kuwa atahakikisha anafanya kazi usiku na mchana bila kujali itikadi, dini na makabila ili kuhakikisha nchi inasonga mbele katika nyanja zote za kimaendeleo.

Akizungumzia maendeleo ya michango mbalimbali kwa ajili ya wathirika wa tetemeko la Ardhi mkoani Kagera Rais Magufuli amesema kuwa mpaka sasa simenti iliyochangwa ni zaidi ya tani 30,600 na mabati zaidi ya elfu 31,000 ambapo wananchi wameshaanza kupewa na kujengea.

Amewahimiza wananchi walioathirika na tetemeko la Ardhi kutotegemea Serikali kuwafanyia kila kitu na badala yake waanze kujenga na watumie msimu huu wa mvua kulima ili kujipatia chakula.

Pia Rais Magufuli amewashukuru na kuwapongeza wahisani waliochangia Maafa ya Kagera na kuwataka kuendelea na moyo huo katika kulijenga Taifa letu.

1 comment:

  1. Hongera mhe.rais kwa kuagiza mikoa,wilaya na halmashauri kupitia upya na kupunguza kodi zisizo za lazima kwa wakulima hasa katika mazao ya biashara kama kahawa ili kuwanufaisha wakulima.Wakulima hii ni fursa kwenu itumieni na hatuna budi kumshukuru kwa moyo wa dhati mhe.rais wetu ndg JP.Magufuli,Ahsante.

    ReplyDelete

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages