Wednesday, December 7, 2016

MSEMAJI WA CCM, OLE SENDEKA ATEULIWA KUWA MKUU WA MKOA WA NJOMBEA, KUFUATIA UTEUZI NA MABADILIKO MADOGO KATIKA WIZARA NA MIKOA YALIYOFANYWA NA RAIS DK. MAGUFULI LEO

Na Bashir Nkoromo, DSM
Rais Magufuli wa Tanzania, Dk. John Magufuli, amemteua Msemaji wa Chama Cha Mapinduzi, Christopher Ole Sendeka kuwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe.

Sendeka anachukua  nafasi iliyoachwa na aliyekuwa Mkuu wa mkoa huo Dk. Rehema Nchimbi ambaye Rais Dk. John Magufuli amemhamishia Mkoa wa Singida kujaza nafasi iliyoachwa na aliyekuwa Mkuu wa mkoa wa Singida Mhandisi Mathew Mtigumwe ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Uvuvi na Mifugo anayeshughulikia Kilimo.

Hayo yametokana na Rais Dk. John Magufuli,  kufanya uteuzi wa Katibu Mkuu mmoja na Mkuu wa Mkoa huyo wa mkoa mmoja na pia kufanya mabadiliko madogo katika Wizara na Mikoa leo, Desemba 7, 2016.

Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Desemba 7, 2016,  imesema, Dk. Magufuli amemhamisha Prof. Faustin Kamuzora kuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais.
kutoka Katibu Mkuu wa Mawasiliano alikokuwa.

Taarifa imesema, Rais Magufuli amemteua Mhandisi Mathew Mtigumwe kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Uvuvi na Mifugo anayeshughulikia Kilimo kuchukua nafasi ya Dk. Frolence Turuka ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na  Job Masima ambaye ameteuliwa kuwa Balozi.

Imesema, Rais Magufuli amemteua Dk. Maria Sasabo kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano na atakuwa akishughulikia Mawasiliano kuchukua  nafasi iliyoachwa wazi na Prof. Faustin Kamuzora ambaye ameteuliwa Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais.

Pia Rais Magufuli amemteua Mhandisi Angelina Madete kuwa Naibu Katibu Mkuu Katika Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Dk. Maria Sasabo aliyeteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia Mawasiliano na pia Rais amemteua Dk. Aloyce K. Nzuki kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii.

Katika hatua nyingine, Rais Magufuli amemteua Dkt. Osward J. Mashindano kuwa Msajili wa Hazina kuchukua nafasi ya iliyokuwa ikishikiliwa na  Lawrence Mafuru ambaye ameondolewa na imeelezwa atapangiwa kazi nyingine
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.