Wednesday, December 21, 2016

ATCL KUPELEKA WANAMICHEZO WA TAASISI YA LOHANA MAHAJAN KISUMU NCHINI KENYA

1
Mwenyekiti wa Taasisi ya Kidini ya Lohana Mahajan Navin Kanabal akitia saini katika moja ya nyaraka wakati taasisi hiyo ilipokabidhiwa tiketi za Shirika la Ndege la ATCL kwa ajili ya safari ya wanamichezo wake kwenda Kisumu Nchini Kenya ambapo keshokutwa jumla ya wachezaji 49 watasafiri kwa kwa ndege ya shirika hilo kwa ajili kushiriki tamasha la michezo ambalo litafanyika nchini humo na kurejea Desemba 27,2016.

Akizungumza katika makabidhiano hayo ya tiketi Mkurugenzi wa Masoko na Maendeleo ya Biashara ATCL Edward Nkwabi ameishukuru taasisi hiyo kwa kutambua na kusafiri kwa ndege za Shirika la Ndege la ATCL kwani itakuwa njia bora na nzuri ya kuanza kujitangaza kimataifa kwa kuanzia katika nchi zetu wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Ameongeza kuwa ATCL itatoa huduma bora kabisa wakati wa safari yao ya Kwenda Kisumu Kenya na Kurudi nchini ili wakati mwingine wasafiri na ndege za ATCL Ameongeza kwamba kwa sasa Ndege za shirika hilo zinatoa huduma ya usafiri wa anga katika viwanja vya Songwe, Bukoba, Mwanza, Kilimanjaro , Zanzibar na Comoro na hapo baadaye wataongeza huduma katika viwanja vya Dodoma na Arusha, Tabora Mtwara pamoja na Mpanda.

Hafla ya makabidhiano ya tiketi hizo imefanyika kwenye Mgahawa wa AKEMI uliopo jengo la Golden Tower jijini Dar es salaam, Katika pichwa wanaoshuhudia tukio hilo ni Mkurugenzi wa Masoko na Maendeleo ya Biashara ATCL Edward Nkwabi wa pili kutoka kulia, James Mbago Meneja Mauzo na Usambazaji, na aliyesimama nyuma ni Katibu wa Taasisi ya Lohana Mahajan Sanjit Ramji.
2
Mwenyekiti wa Taasisi ya Kidini ya Lohana Mahajan Navin Kanabal akipokea tiketi kutoka kwa Mkurugenzi wa Masoko na Maendeleo ya Biashara ATCL Edward Nkwabi kwa ajili ya wanakikundi wenzake 48 kwa ajili ya safari ya kwenda na kurudi Kisumu nchini Kenya kwa ajili ya Tamasha la Michezo litakalofanyika nchini humo.
3
Mkurugenzi wa Masoko na Maendeleo ya Biashara ATCL Edward Nkwabi akimkabidhi tiketi Meneja wa timu ya Lohana Mahajan Bi. Sona Thakrar.
4
Mkurugenzi wa Masoko na Maendeleo ya Biashara ATCL Edward Nkwabi akiwa katika picha ya pamoja na maofisa wenzake kutoka shirika la ndege la ATCL baada ya kumalizika kwa hafla hiyo.
Share:

KUCHAGUA LUGHA

IDADI YA WATU AMBAO HUTEMBELEA BLOGU HII

KUMBUKUMBU ZA POSTI ZOTE

JISAJILI UPATE TAARIFA KWA EMAIL

Jisajili ili upate taarifa kwa email

Google+ Followers

Powered by Blogger.