SHIRIKISHO LA ELIMU YA JUU WAKUTANA NA MBUNGE JASMINE TUSEMWA.


Displaying 20161030_155806_001.jpg
MBUNGE WA VITI MAALUMU MH. JASMINE TISEKWA BUNGA AKIZUNGUMZA NA VIONGOZI WA SHIRIKISHO LA ELIMU YA JUU.


Viongozi wa Shirikisho la Wanafunzi wa  Elimu ya juu kwa mara ya kwanza leo wamekutana na mbunge wa viti maalum kupitia vyuo vikuu Mhe Jasmine Tisekwa Bunga katika hoteli ya Oasis Mjini Morogoro.ambaye.

Wakati wa mazungumzo na mbunge huyo viongozi wa Shirikisho Taifa akiwemo KaTIBU Msaidizi Ndugu Daniel Zenda walizungumza mambo mbalimbali yanayoizzunguka jumiya hiyo.

Pia Shirikisho limewasilisha hoja mbalimbali pamoja na mapendekezo yenye maslahi ya Wanafunzi kwa ujumla yanayotokana na changamoto zilizopo katika vyuo vya elimu na sekta ya elimu kwa ujumla zitakazo wasilishwa bungeni kupitia  "Part cocus ya CCM", kamati za Bunge na kipindi cha Bunge hasa kipindi cha maswali na majibu. 

Akizungumza baada ya kumaliza kwa kikao hicho Ndugu Zenda alisema kikao kimeisha salama na kilikuwa ana mafanikio makubwa.

“Kikao kilifanyika na kumalizika vizuri  tunamshukuru mungu kilikuwa na mafanikio makubwa maana tuliazimia (Resolutions ) mambo yenye tija kwa wanafunzi na maslahi kwa lengo la kukijenga chama cha mapinduzi ili kiendelee kuaminiwa na kushika dola.” Alisema Zenda na kuendelea:-

“Tunatambua  shirikisho linaendelea kufanya kazi zake za kila siku na kila wanachama wa CCM na viongozi  wawajibike kwa nafasi zao,” alisema Zenda.

Hivyo Changamoto za Mikopo na nyingine zitawasilishwa na Viongozi Wa Mikoa kwa Utaratibu zilizo wekwa na Shirikisho.

0 comments:

Post a Comment

Mdau, Uwanja huu ni wako, Toa maoni yako yasaidie kujua wewe unafikiri nini kifanyike kuboresha zaidi maisha ya Watanzania. Maoni yako yasilenge kuchochea mtafaruku katika jamii, kisiasa, kidini, kikabila au kijinsia. Mawasiliano yetu:- simu +255 (0) 712 498008, Email: nkoromo@gmail.com.
Bashir Nkoromo
Msimamizi Mkuu, Blog ya Taifa ya CCM.