WAZIRI MWIGULU AFANYA MAZUNGUMZO NA WATENDAJI WA SHIRIKA LA UMOJA WA MATAIFA LA KUPAMBANA NA DAWA ZA KULEVYA NA UHALIFU (UNODC)

 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, akizungumza na watendaji wa  Shirika la Umoja wa  Mataifa la Kupambana na Dawa za  Kulevya na Uhalifu (UNODC),  Kaitlin Meredi (kulia) na  Johan Kruger (kushoto), walipomtembelea ofisini kwake,jijini Dar es Salaam, leo. Ziara hiyo ikiwa na lengo la kujadili njia muafaka za kukabiliana na biashara, matumizi na athari za dawa za kulevya kwa jamii. 
Mkuu wa Kitengo cha Kupambana na Biashara Haramu ya Dawa za  Kulevya kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Kupambana na Dawa za Kulevya na Uhalifu(UNODC), Johan Kruger(kushoto), akiagana na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, baada ya mazungumzo yao, walipomtembelea ofisini kwake kwa ajili ya kuzungumzia juhudi mbalimbali za  kupambana na biashara haramu ya Dawa za Kulevya.Kulia ni Mratibu  wa Kupambana na Uhalifu wa Majini, Kaitlin Meredith

0 comments:

Post a Comment

Mdau, Uwanja huu ni wako, Toa maoni yako yasaidie kujua wewe unafikiri nini kifanyike kuboresha zaidi maisha ya Watanzania. Maoni yako yasilenge kuchochea mtafaruku katika jamii, kisiasa, kidini, kikabila au kijinsia. Mawasiliano yetu:- simu +255 (0) 712 498008, Email: nkoromo@gmail.com.
Bashir Nkoromo
Msimamizi Mkuu, Blog ya Taifa ya CCM.