WAKAZI ARUSHA WAWASHANGAA CHADEMA KUINGILIA MAJUKUMU YA MHESHIMIWA MRISHO GAMBO

Image result for PICHA MRISHO GAMBO


Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mheshimiwa Mrisho Gambo 

Na:Nasri Bakari 0713 311 300
Baada ya kuteuliwa na Mheshimiwa Rais kuwa mkuu mpya wa mkoa wa Arusha na hatimaye jana kuapishwa Ikulu jijini Dar es salaam Mheshimiwa Mrisho GamboWAKATI Mkuu mpya wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo akiapishwa jana Ikulu, Dar es Salaam, baadhi ya wananchi wa Jiji la Arusha wameshangazwa kuona viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wakidai kuwa anaingilia kazi za jiji hilo.

Akiongea na Ccm blog mmoja wa wakazi wa Arusha , ndugu Ismail Isaac alisema "tatizo ni siasa za chuki kati ya Chadema dhidi ya RC Gambo na kutaka wamuache afanye kazi kwani wananchi wanamkubali, hivyo kama chama hicho cha upinzani hakimkubali, kitajua chenyewe"

“Wananchi wanahitaji maendeleo sasa huu ushawishi wa Chadema kwenda kwa wenyeviti wa mitaa unatoka wapi? Huyu Gambo anafanya kazi, sasa vikwazo ni vya nini?” alisema huku akisisitiza.

Mwananchi huyo wa jiji hilo aliwashangaa madiwani wa Chadema wanaotaka siasa za chuki ambazo wananchi hawapo tayari kuzikubali. Kwa upande wake, Katibu Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), mkoa wa Arusha, Shaaban Mdoe, alisema Arusha kuna siasa nyingi hivyo ni vyema viongozi wakatimiza majukumu yao ya kikazi na kutokatishwa tamaa

0 comments:

Post a Comment

Mdau, Uwanja huu ni wako, Toa maoni yako yasaidie kujua wewe unafikiri nini kifanyike kuboresha zaidi maisha ya Watanzania. Maoni yako yasilenge kuchochea mtafaruku katika jamii, kisiasa, kidini, kikabila au kijinsia. Mawasiliano yetu:- simu +255 (0) 712 498008, Email: nkoromo@gmail.com.
Bashir Nkoromo
Msimamizi Mkuu, Blog ya Taifa ya CCM.