Sunday, July 10, 2016

WAZIRI MKUU WA INDIA AONDOKA LEO

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na mgeni wake Waziri Mkuu wa India Narendra Modi katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Waziri Mkuu huyo ameondoka baada ya kufanya shughuli mbalimbali leo ikiwemo mazungumzo ya faragha na Mwenyeji wake Rais Dk. Magufuli na baadaye kusaini mikataba ya miradi ya kiuchumi baina ya  Tanzania na India.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Waziri Mkuu wa India Narendra Modi kabla ya kuondoka katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili nchini. 
 Waziri Mkuu wa India Narendra Modi akipungia mkono vikundi vya utamaduni vilivyokuwa vikitoa buradani katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili nchini.


 Waziri Mkuu wa India Narendra Modi na Rais Dk. Magufuli wakiwa na watoto wa Kitanzania wenye asili ya Kiasia kabla ya Waziri Mkuu huyo kuondoka Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

 Waziri Mkuu wa India Narendra Modi akiagana na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan kabla ya kuondoka jijini Dar es Salaam.

 Waziri Mkuu wa India Narendra Modi akishukuru kabla ya kuondoka  baada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili nchini.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wafanyakazi wa kitengo cha mizigo katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa JINIA  jijini Dar es Salaam mara baada ya kumsindikiza mgeni wake Waziri Mkuu wa India Narendra Modi. PICHA NA IKULU
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.