Naibu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu
wenye Ulemavu Dkt. Abdallah Possi, (wapili kulia), akionyesha Ripoti ya Matokeo ya Utafiti wa
Utumikishwaji wa Watoto Tanzania wa Mwaka 2014. Uzinduzi huu umefanyika Julai
20, 2016 jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango.
Mkurugenzi
Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa akitoa maelezo ya
utangulizi kuhusu Utafiti wa Utumikishwaji wa Watoto Tanzania wa Mwaka 2014
katika uzinduzi wa matokeo hayo uliofanyika jijini Dar es Salaam katika ukumbi
wa Wizara ya Fedha na Mipango.
Mwakilishi
wa Shirika la Kazi Duniani nchini Tanzania, Azfar Khan akizungumza jijini
Dar es Salaam katika uzinduzi wa Matokeo ya Utafiti wa Utumikishwaji wa Watoto
Tanzania wa Mwaka 2014. (PICHA ZOTE
NA EMMANUEL GHULA)
NA MWANDISHI WETU
UTUMIKISHWAJI
wa Watoto bado ni tatizo kubwa nchini ambapo kati ya watoto watatu wenye umri
wa miaka 5 - 17, mtoto mmoja anafanya kazi ambazo ni hatarishi katika maisha
yake kiafya, kimwili na kisaikolojia.
Akizungumza
katika uzinduzi wa Ripoti ya Matokeo ya Utafiti wa Utumikishwaji wa Watoto
Tanzania wa Mwaka 2014, Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge,
Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Dkt. Abdallah Posi amesema tatizo la
utumikishwaji wa watoto bado ni kubwa hapa nchini na hivyo ni wajibu wa jamii
kuwekeza katika elimu badala ya kuwaajiri au kuwatumikisha watoto.
“Utumikishwaji
wa watoto bado ni tatizo kubwa duniani kote si Tanzania pekee, kwani kwa mujibu
wa takwimu za Shirika la Kazi Duniani (ILO), asilimia 11 ya watoto wote duniani
(watoto milioni 264) wenye umri wa miaka 5 – 17 wanatumikishwa kwenye ajira za
aina mbalimbali,” amesema Dkt. Posi.
Dkt.
Posi amesema kwa mujibu wa ripoti ya utumikishwaji wa watoto Tanzania wa mwaka
2014/15, watoto wenye umri wa miaka 5 – 17, watoto milioni 4.2 ambao ni sawa na
asilimia 28.8 wanatumikishwa katika kazi mbalimbali za kiuchumi.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa
amesema utafiti huu umebainisha kuwa, watoto wanafanya kazi zaidi katika sekta
za Kilimo, Misitu na Uvuvi ambazo zinaajiri asilimia 92.1 ya watoto wote
wanaojishughulisha na shughuli za kiuchumi.
Dkt.
Chuwa ameongeza kuwa watoto hutumia zaidi ya nusu ya muda wao (asilimia 58.8)
wa siku kujihudumia na usafi binafsi ambapo wasichana wameonekana kutumia
asilimia 59.2 na wavulana hutumia asilimia 58.3 kujihudumia.
Aidha,
shughuli za kujisomea kwa watoto ni asilimia 15.5 ambapo wavulana wanatumia
muda mrefu zaidi kujisomea kwa asilimia 16.4 na wasichana hutumia asilimia 14.6
kujisomea
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇