Sunday, July 10, 2016

RIDHIWANI KIKWETE ASAIDIA WAGONJWA WA MACHO

Daktari akimsikiliza mgonjwa na kumfanyia vipimo huku Mbunge jimbo la Chalinze Mkoa wa Pwani Ridhiwani Kikwete (mwenye Barghashia) akisubiria zamu yake kupata vipimo huku akifatilia zoezi linavyoendeshwa. 
Daktari akimsikiliza Bibi ayefika kupata matibabu ya macho.
sehemu ya kupata dawa baada ya kufanyiwa vipimo.

Mbunge Ridhiwani akiwa chumba cha operasheni kuangalia jinsi operesheni ya macho inavyofanywa.picha zote na  Omary Mngindo.


Na Omary Mngindo, Chalinze
MBUNGE wa Jimbo la Chalinze Halmashauri ya Chalinze Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani Ridhiwani Kikwete amewezesha zoezi la upimaji wa macho kwa wakazi jimboni humo na kupatiwa miwani kwa wakazi zaidi ya 2,000.

Zoezi hilo ambalo limelenga kuwapatia huduma hiyo wananchi hao ambao wanakabiliwa na tatizo hilo huku aakikosa uwezo wa kupata huduma kutokana na hali ya kipato, ambapo Taasisi ya Bilal Muslimu Mission ya jijini Dar es Salaam imeendesha zoezi hilo katika Kata ya Bwilingu ambapo mamia ya wananvhi wakijitokeza kupata huduma.

Akizungumza na waandishi wa habari, Ridhiwani alisema kwamba alikutana na viongozi wa taasisi hiyo na kufanya nao mazungumzo nao ili wafike kuwapayia huduma ya kuwapima macjo na kupewa miwani ambapo zoezi hilo limefanyika, wananchi wamepimwa na kupewa ushauri, mtiba na wemgine kupewa miwani.

"Leo sio siku ya kuzungumza sana kwani nina furaha kubwa ya kuona wananchi wamepatiwa huduma ya vipimo, kupatiwa ushauri, kutibiwa macho na wengine kupatiwa miwani, pia nimewaomba viongozi wa Bilal kuendelea kutoa huduma ndani ya jimbo lengo wote wafaidike na huduma," alisema Ridhiwani.

Wananchi wakiwa katika foleni ya kusubiri kupata huduma ya kupima macho.
wananchi wakipata maelekezo kutoka kwa mtoa huduma.

Kwa upande wake Mratibu wa Taasisi ya Muslimu Ain Sharifu alisema kuwa tangu wafike kuanza kuwapatia huduma hiyo wananchi wamejitokeza kwa wingi kupata huduma, wamewashauri, wamewapatia tiba pia miwani kwa waliotakiwa kupatiwa na kuwa zaidi ya watu 2,000 wamenufaika na huduma hiyo.

"Tunashukuru kwani katika kipinfi chote cha siku tatu za zoezi wananchi wametupatia ushirikiano mkubwa, taasisi yetu pia inayoa huduma mkoani Morogoro, tunakuhakikishia Mbunge Ridhiwani kwamba tutaendelea kuwapatia huduma, tutawaleta mafaktari wetu ili waendelee kuwapatia huduma zaidi," alisema Sharifu.

Awali akizungumza katika hafla hiyo ya ufungaji wa utoaji wa huduma hiyo, diwani wa Kata ya Bwilingu Lucas Lufunga alisema kuwa katika kipindi chote cha zoezi wananchi wameonesha ushirikiano mkubwa katika mchakato huo.
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.