RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE AKUBALI OMBI LA RAIS FILIPE NYUSI WA MSUMBIJI KUSHIRIKI MAZUNGUMZO YA AMANI NCHINI MSUMBIJI

Rais Mstaafu Dk. Jakaya Mrisho Kikwete amepokea ujumbe maalum kutoka kwa Rais Filipe Nyusi wa Msumbiji.

Ujumbe huo uliwasilishwa jana jijini Dar es Salaam na Mjumbe Maalum wa Rais Nyusi Meja Jenerali Mstaafu Mariano de Araujo Matsinhe ambaye aliongozana na Mshauri wa Diplomasia wa Rais Nyusi, Kanali Manuel Mazuze, Balozi wa Msumbiji nchini Tanzania Monica Patricip Clemente Mussa na Afisa wa Ubalozi wa Msumbiji nchini Rachide Usualle.

Katika Ujumbe huo, Rais Nyusi amemuomba Rais Mstaafu Dk. Jakaya Kikwete kushiriki mazungumzo ya amani nchini Msumbiji, ambapo Dk. Kikwete amekubali.
Mheshimiwa Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katika mazungumzo na ujumbe wa Rais Filpe Nyusi uliofika kuwaslisha ujumbe maalum jijini Dar es Salaam jana

0 comments:

Post a Comment

Mdau, Uwanja huu ni wako, Toa maoni yako yasaidie kujua wewe unafikiri nini kifanyike kuboresha zaidi maisha ya Watanzania. Maoni yako yasilenge kuchochea mtafaruku katika jamii, kisiasa, kidini, kikabila au kijinsia. Mawasiliano yetu:- simu +255 (0) 712 498008, Email: nkoromo@gmail.com.
Bashir Nkoromo
Msimamizi Mkuu, Blog ya Taifa ya CCM.