LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jun 6, 2016

CCM: UKAWA WAKIMCHAFUA RAIS DK. MAGUFULI TUTAKULA NAO SAAHANI MOJA KUMTETEA

NA BASHIR NKOROMO
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM),  kimeonya  vikali  juu ya  mkakati wa  viongozi wa UKAWA,  wa kufanya ziara   mikoani, katika kile ambacho wanakiita ni kwenda kuishitaka serikali  ya awamu ya tano  chini ya  Rais Dk. John Magufuli  kwa wananchi.

Aidha CCM  kimesema, daima hakitavumilia  juu ya jambo lolote  ambalo litaonekana kuwa na nia ovu ya kumchafua Rais Dk. Mafuli  na  kitakula sahani moja  na UKAWA  katika kampeni hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari, jijini Dar es Salaam, jana, Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka, alisema, wamesikitishwa  na kauli  zinazotolewa na  wapinzani  ya kupinga  kasi ya Rais Dk. Magufuli hususan katika dhama yake ya utumbuaji majipu, kubana bajeti na matumizi ya serikali pamoja na  kuzitafutia ufumbuzi  changamoto za wananchi katika sekta mbalimbali.

Sendeka alisema, upo mkakati mchafu ambao wapinzani wamekuwa wakipanga  kwa nia mbaya ya kutaka kuchafua taswira ya Rais Dk. Magufuli , mkakati  ambao  amedai  hauwezi kuungwa mkono na wananchi.

Alisema, tangu Mei 16 mwaka huu baada  ya Kikao cha Kamati Kuu ya CHADEMA, habari za mwanzo zilianza kuandikwa katika vyombo mbalimbali vya habari juu ya yaliyojiri katika mkutano huo.

Alisema,   mkakati   huo  unaegemea katika kuandaa umma kwa kile kinachoitwa kwenda kumshitaki Rais Dk. Magufuli kwa wananchi.

“Kwamba Serikali ya  Rais Dk. Magufuli  inaidaiwa kuendesha nchi kifashist na inalenga kuipeleka nchi  katika utawala  wa kidikteta ambao haujazoeleka katika nchi yetu,”alisema Sendeka.

Alisema, kipindi cha nyuma moja ya mambo ambayo yalikuwa yakipigiwa kelele na vyama vyote ni ufisadi, rushwa  na  suala la  serikali kutokuwa na maamuzi, ambapo baada ya uchaguzi  mkuu uliopita,  baada ya Rais Dk. Magufuli kuchaguliwa  amesimama kidete kupambana na  mambo hayo licha ya kwamba   yapo katika, ilani ,  sera za msingi na  kiapo cha  uanachama cha CCM.

“Wenzetu mara baada ya kumpata mgombea wao  (Edward Lowassa), ujasili wa kuzungumzia rushwa na ufisadi ulipungua. Kwa sababu ambazo  kila mtanzania anajua kwamba ni kwanini wamekosa utashi wa kuendelea kulikemea suala hilo la rushwa , ufisadi na ubadhirifu wa mali za umma,”alisema Sendeka.

Alisema, baada ya Rais Dk. Magufuli, kuingia Ikulu, mapambayo dhidi ya mambo hayo ameyafanya kwa kasi ya aina yake, ikiwa ni pamoja na kuziba mianya  ya rushwa, kuziba mianya ya upotevu wa fedha za serikali, kubana matumizi kwa kufuta   bajeti kubwa za Sikukuu, kufuta safari za nje pamoja na wakati mwingine kuelekeza fedha  katika maeneo  ambayo yanamatatizi makubwa.

Alise, Rais Dk. Magufuli alichokuwa anafanya ni kumalizia ngwe ya mwisho ya bajeti ya mwaka wa fedha 2015/16 na kwamba atafanya vizuri zaidi baada ya bajeti ya mwaka wa fedha 2016/17 kupitishwa.

“Katika  mapambano hayo,  ambayo  rais ameyafanya kwa utashi mkubwa,  tunajua kwamba yamegusa watu wengi . Hakuna mashaka kwamba katika nchi hii tayari kuna watu ambao wametengeneza utajiri wa muda mfupi ambao  unatia ukakasi  unaoweza kumuudhi mtu yoyote mwenye mapenzi na nchi hii,”alisema Sendeka.

Alisema  utendaji huo ulifanya  kupokea sifa nyingi  zilizoelekezwa kwa Rais juu ya utendaji wake, lakini baada ya kikao cha Kamati Kuu ya CHADEMA,  walibaini wazi bila mashaka kwamba anayoyafanya Rais Dk. Magufuli yanapandisha chati ya CCM kwenda juu. Kwa sababu serikali iliyopo madarakani  ndiyo inayokijengea chamas uhalali na uhalali wa chama chochote unsajengwa na utendaji wa serikali iliyopo madarakani.

“Serikali  iliyopo madarakani isipo tekeleza matarajio ya wananchi, uhalali wake haupo. Vitendo vya Rais Dk. Magufuli, hakuna mashaka kwamba watanzania  wameunga mkono na Dunia imeunga mkono.  Hata umoja wa mataifa kupitia Shirika la Maendeleo (UND) imeunga mkono uwajibikaji huo, katika  mapambano ya rushwa ,  ukusanyaji mapato na nidhamu ya uwajibikaji kwa watumishi wa umma,”alisema Sendeka.

Alisema, inashangaza kuona kwamba CHADEMA wanadai suala la kupambana na rushwa na ufisadi  Rais Dk. Magufuli amepora kwao na kusahau kwamba , ajenda hiyo ilikuwa ni ya CCM na TANU.

“Kilicho fanyika ni kumpata kada ambaye anaweza kusimamia na kutekeleza hayo, jambo ambalo limeanza kuwafanya wapinzani kuamini kwamba  itaua  upinzani, na kwamba hofu yao ni uwezekano wa kupoteza  wabunge wengi katika uchaguzi mkuu wa 2020 ni mkubwa,”alibainisha msemaji huyo.

Alisema baada ya kufanya tathimini hiyo ndipo walipokubariana kwenda kwa wananchi  wakiwa na ajenda  ya kupotosha umma juu ya utendaji  wa Rais Dk. Magufuli na serikali yake.

“Walianza na kampeni ya rais ya utumbuaji wa majipu na wao kupitia kwa mgombea wao wa urais Lowassa kisha kwa mwenyekiti wa CHADEMA , Freeman Mbowe, walikemea  ajenda hiyo kwamba inaukiukwaji wa haki za binadamu.

Kwamba unapokwenda bandarini nakukuta makontena 2000 au 3000 hayajalipiwa kodi unamuacha huyo Kamashna  na wasaidizi wake  na kwamba hiyo ndiyo haki ya binadamu?” alihoji Sendeka.

Alisema  viongozi hao pia waliponda kwamba serikali ya Rais Dk. Magufuli inatanguliza vitendo kuliko fikra.
“Hivi jamani, umemkuta mtu na kila  dalili za kufanya ufisadi, unamuacha na kuanza kufikiria jambo la kufanya.

Serikali ya Magufuli inasema kaa pembeni, jitetee kisha hatua  zaidi zinachukulia .Hii ni kwa nia njema ya kueta maendeleo ya nchi kwa kutumia  vyanzo vya mapato yetu, kutoa huduma muhimu zinazostahili kwa wananchi.

Na kazi hiyo ameifanya kwa ufanisi mkubwa kwa muda mfupi aliokaa katika uongozi,”alibainisha Sendeka.

Aliongeza “Sasa haya yamewaudhi. Walijaribu kupima kina cha maji wamebaini kwamba hawayawezi na wamebaini kwamba watanzania wote wamechoka na wanaunga mkono hatua hizi za rai,”

Sendeka alishangazwa na wapinzani  kulalamikia hatua ya Rais Dk. Magafuli kutumbua majipu   kwamba ni udikteta na ufashisti wakati rais ania njema ya kutetea wanyonge na maslahi mapana  ya taifa.

Alisema binafsi anamuunga mkono Lowassa kwa kauli yake aliyoitoa hivi karibuni  kwamba, kazi yake kubwa sasa  ni kukigeuza CHADEMA kutoka kuwa katika kikundi cha wanaharakati na kuwa chama kamili.

“Najiuliza kama miaka 20 zaidi ya uwepo  wa CHADEMA hakikuweza kubadilika kutoka katika kikundi cha wanaharakati mpaka Lowassa alipo kikuta na kutaka kukibadilisha ndani ya miaka minne ijayo  kiweze kuwa chama kamili cha siasa nina uhakika muda huo hautoshi,” alisema Sendeka.

Aliongeza, ”Lakini najiuliza  kama  Magufuli anatumbua majibu wapinzani wanadai ni dikteta na fashist. Magufuli  anaziba mianya ya rushwa   wanachukia. Najiuliza wametumwa nanani? Kumwakilisha nani? Kutetea maslahi ya nani? Na nani kawafadhili?
Alisema  ni dhahiri anayetetea ufisadi  anawasemea waliotumbuliwa na ambao mianya yao ya rushwa imezibwa.

Sendeka alisema, wakati ufusadi  ulivyo kuwa ukifanyika katika sekta muhimu, wapinzani hawakuacha Bunge wala vikao na kwenda kuitisha mikutano kwa wananchi na kuwaambia kwamba bandari na TRA kuna ufisadi.

“Wakati wa kashfa ya ukwepaji wa kodi ya sukari hakuna aliyetoka kwenda kwa wananchi kuitisha mikutano  au  kuingia barabarani    kuandamana kwa sababu kodi haijalipwa. Wakati wa kashfa ya Escrow,  hakuna chama kilicho funga safari kwenda mikoani kuitisha mikutano na kuwaeleza wananchi  kwamba kuna ufisadi huo,”alisema Sendeka.

Alisema, inshangaza kuona wakati serikali inajitahidi kupambana na changamoto  zinazowakabili wananchi,  wapinzani wanajipanga kwenda mikoani kupinga hatua hizo kwa kile wanachokiita kushtaki serikali kwa wananchi.
.
“Dhamira ya wenzetu sasa ni kujitahidi  kutumia nguvu zao na zawale  wanaowatuma kuchafua jina la Dk. Magufuli bila kuelewa kwamba Watanzania  hasa wanyonge wataendelea  kutumia jina la Rais huyu kama alama kuu na muhimu , katika mapambano dhiti ya ukiritimba, ufisadi, na viongozi  na watendaji wanaokubali kufanya kazi ya ukuwadi kwa manufaa  yao binafsi huku wakiyaweka pembeni maslahi ya taifa,” alisema Sendeka.

Alisema CCM haipingi  ziara hizo za viongozi, lakini  daima hakitavumilia ikiwa mikutano yao italenga katika kumchafua rais.

“Wakijaribu kuchafua rais,  watakapo CCM nayo itakanyaga pia. Watakapo ondoa  mguu wao nasisi tunaweka  mguu wetu ili kuwaeleza ukweli wananchi juu ya kazi kubwa inayofanywa na serikali. Tunawasemaji wengi  na tunauwezo wa kufika popote,” alisema Sendeka.

Aliongeza, ”Watanzania watapima, kauli ya watu wanaotetea mafisadi, wakwepa kodi na wala rusahwa na CCM inayotetea  wananchi wanyonge  ili waweze kufaidi matunda ya nchi yao,”

Alisema, kama hoja zao ni hizo,  za kumchafua Rais Dk. Magufuli CCM inawaonea huruma,  na wasifiriki watanzania walio timamu watawaunga mkono.

“Siyo tu kwamba watanzania hawatawaunga mkono, bali watawashangaa na heshima yao itashuka. Watanzania wanaakili, hawawezi kutetea wezi  wakati rais anafanya kazi nzuri ya kuwatetea,”


No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages