Saturday, May 7, 2016

RAIS MAGUFULI ATUNUKU KAMISHENI MAAFISA WAPYA 586 WA JWTZ,ATANGAZA KUKAMATWA KWA WAFICHA SUKARIRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli leo Jumamosi tarehe 07 Mei, 2016 amewatunuku Kamisheni Maafisa wapya 586 wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kundi la 58/15 waliomaliza mafunzo yao katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli (TMA) Mkoani Arusha.
Maafisa hao wapya wa Jeshi walianza kozi yao tarehe 04 Mei, 2015 na wamepewa cheo cha Luteni usu.
Kati ya maafisa wapya waliohitimu kozi yao leo, 80 ni madaktari na 6 ni marubani wa ndege waliopata mafunzo yao katika nchi tatu ambazo ni Tanzania, Uganda na Afrika Kusini.


Share:

KUCHAGUA LUGHA

IDADI YA WATU AMBAO HUTEMBELEA BLOGU HII

KUMBUKUMBU ZA POSTI ZOTE

JISAJILI UPATE TAARIFA KWA EMAIL

Jisajili ili upate taarifa kwa email

Google+ Followers

Powered by Blogger.