Friday, April 15, 2016

NAPE: MADIWANI WAZINGATIE VIWANJA VYA MICHEZO KATIKA KILA MPANGO MJI WA MAKAZI YA WATU


 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akizungumza na washika dau wa Habari, Utamaduni Sanaa na michezo wa mkoa wa Mara ikiwa sehemu ya ziara yake ya kukutana na wadau hao wakiwemo watumishi wa serikali .


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye leo ameendelea na ziara yake katika mkoa wa Mara na Shinyanga ambapo alikutana na Watumishi na wadau walio chini ya Wizara yake.
 Waziri Nape alipokea taarifa zaSerikali pamoja na maoni ya wadau mbali mbali ambapo aliwapongeza kwa kuwa na maoni mazuri na kusisitiza Wizara yake itakuwa karibu nao na kufanya ziara za mara kwa mara katika kuhakikisha mambo waliyopanga yanafanikiwa.

Waziri Nape aligusia mambo mbali mbali ya msingi wakati akiongea na washika dau waliokuwa chini ya wizara yake na kusisitiza kuwa Madiwani wanaoshiriki katika mipango mji wanatakiwa kuzingatia kutenga viwanja vya michezo kwa watoto wa eneo husika pia alishauri mikoa kuanzisha vituo vya utamaduni wa mkoa ambavyo vitakuwa vyanzo vya kutunza utamaduni lakini pia sehemu ya kuvutia utalii akitolea mfano kituo cha Bujora mkoani Mwanza.

Mhe. Nape pia aliwataka Makatibu Tawala za Mikoa  wajenge utamaduni wa kukutana na vyama vya michezo kwani wao ni walezi muhimu wa vyama hivyo.


 Sehemu ya washika dau waliohudhuria kikao cha Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa mkoa Mara.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye ambaye pia ni Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi wa CCM Mhe. Nape Nnauye akisaini kitabu cha wageni katika Ofisi ya CCM mkoa wa Mara.


 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye ambaye pia ni Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi wa CCM Mhe. Nape Nnauye akizungumza na viongozi wa CCM katika Ofisi ya CCM mkoa wa Mara.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye ambaye pia ni Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi wa CCM Mhe. Nape Nnauye akizungumza na viongozi wa CCM katika Ofisi ya CCM mkoa wa Mara ambapo aliwataka viongozi hao kutembea kifua mbele kwani ilani waliyoiandaa inatekelezwa vyema.
 Sehemu ya uwanja wa mpira wa Kambarage mkoani Shinyanga.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akifafanua jambo kwenye uwanja wa mpira wa Kambarage mkoani Shinyanga.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akizungumza na wadau kwenye uwanja wa mpira wa Kambarage mkoani Shinyanga.

 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea mitambo ya kurusha matangazo ya TBC mkoani Shinyanga.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akizungumza na watumishi wa serikali pamoja na wadau wa sekta ya habari, utamaduni, sanaa na michezo wa mkoa wa Shinyanga .
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.