Monday, April 18, 2016

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AZINDUA MBIO ZA MWENGE WA UHURU MKOANI MOROGORO LEO

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwasha  Mwenge wa Uhuru na kuzindua rasmi mbio za Mwenge wa Uhuru Mwaka 2016 leo Aprili 18, 2016  sherehe iliyofanyika katika uwanja wa Jamhuri Mkoani Morogoro. Kulia ni Waziri wa Uwezeshaji Ustawi wa Jamii, Vijana, Wanawake na Watoto -  Zanzibar Mhe. Modelin Kastiko.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimkabidhi Mwenge wa Uhuru kiongozi wa mbio za Mwenge kwa mwaka 2016  George Jackson Mbijima kutoka mkoa wa Mbeya kwa ajili ya kukimbiza mwenge huo katika Mikoa na wilaya zote za Tanzania.

 Vijana wa halaiki wakiwakaribisha wakimbiza Mwenge wa Uhuru kuingia uwanjani kwenye sherehe za uzinduzi wa mbio za Mwenge , Uwanja wa Jamhuri mkoa wa Morogoro

Vijana sita watakaokimbiza Mwenge wa Uhuru nchi nzima wakiingia kwenye uwanja wa Jamhuri kwa ukakamavu mkubwa.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akizungumza na Waziri wa Ofisi ya Rais ,TAMISEMI,utumishi na Utawala bora,George Simbachawene.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI


Share:

KUCHAGUA LUGHA

IDADI YA WATU AMBAO HUTEMBELEA BLOGU HII

KUMBUKUMBU ZA POSTI ZOTE

JISAJILI UPATE TAARIFA KWA EMAIL

Jisajili ili upate taarifa kwa email

Google+ Followers

Powered by Blogger.