Tuesday, April 12, 2016

BABATI WAIPONGEZA CCM KWA KUMWAMINI NA KUMUUNGA MKONO RAIS DK. JOHN MAGUFULI KATIKA UPASUAJI MAJIPU

Rais Dk. John Magufuli
NA BASHIR NKOROMO, BABATI
WANANCHI mkoani Manyara wamekipongeza Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kumwamini na kumuunga mkono Rais Dk. John Magufuli, kwenye jitihada zake za kurudisha nidhamu ya watumishi wa sekta za umma tangu alipoingia madarakani Novemba, 2015.

Pia wamekipongeza kwa kutambua uwezo alionao Christopher Ole Sendeka, ambaye ameteuliwa hivi karibuni na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Jakaya Kikwete, kuwa Msemaji wa Chama hicho ngazi ya Taifa.

Wakizungumza na kwa nyakati tofauti jana, wananachi hao wa wilaya ya Babati vijijini walisema wao ni mashuhuda wa namna CCM inavyoendelea kuimarika tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa mwaka jana.

Walisema wanaamini ukomavu wa kidemokrasia ulioko ndani ya CCM ambao ulitumika kumpata Dk. John Magufuli ambaye aliipeperusha vema bendera ya chama kwenye uchaguzi huo uliokuwa wa kihistoria ni moja ya sababu za kurudi kwa uhai wa chama.

Paul Deemay mkazi wa kijiji cha Bashnet wilayani humo, alisema uhai huo umetoa matumaini mapya kwa wananchi kukiamini Chama hicho, kuwa ndicho chenye uwezo wa kuivusha Tanzania kwenda kwenye uchumi endelevu wa viwanda.

Alisema CCM ina utajiri wa viongozi makini wenye maono, sifa ambazo zinaendelea kudhihirika kutokana na kuwa na serikali yenye msimamo iliyoundwa Dk. Magufuli, ilani ya chama iliyokusudiwa kupambana na ufisadi na ukuzaji uchumi kwa kasi ya ajabu.

Naye Mary Focus, ambaye ni Mwanafunzi wa chuo cha kodi cha Dar es Salaam na mkazi wa Babati, alisema anatarajia mambo makubwa kwa Awamuhii ya Tano inayoongozwa na Dk. Magufuli asiyependa mzaha kwenye utumishi za umma.

Alisema Ole Sendeka aliyeteuliwa kuwa Msemaji Mkuu wa CCM hivi karibuni ni mtu mchapakazi na kwamba mkoa wa Manyara unajivunia mafanikio yake kwenye siasa hivyo CCM imefanya chaguo sahihi kumpa jukumu hilo.

“Ole Sendeka anastahili kushika nafasi aliyokabidhiwa na CCM, ni mchapakazi na sisi watu wa Manyara na Tanzania kwa ujumla tu mashahidi katika hilo naamini atakitetea chama kwa akili na busara zake zote,”alisema Mary.
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.