Saturday, February 20, 2016

WANAHABARI PAMOJA NA WASANII WATAKIWA KUJIUNGA NA KUWA NA WAWAKILISHI WAO.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akizungumza na waandishi wa habari, wasanii, pamoja na madereva walioshiriki kwenye kampeni zake za kugombea Urais ambapo aliwaambia kuwa hamna kitu kizuri kama kuwa wamoja kwenye kila jambo hivyo aliwataka kwa nafasi zao kujiunga na kuwa na wawakilishi ambao watafikisha moja kwa moja mambo yao kwa viongozi wa juu.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na makundi mbali mbali yaliofanikisha kazi nzuri wakati wa kampeni ambapo aliwataka wasanii wa Tanzania Bara kushirikiana vizuri na wasanii wa Visiwani Zanzibar .
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza mbele ya waandishi wa habari na wasanii ambapo aliwaambia Wasanii hao kuwa Serikali inatambua mchango wa kazi zao katika jamii na kuwaahidi atapanga siku maalum azungumze nao ili kuona namna gani changamoto zao zinaweza kutatuliwa.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akizungumza mbele ya waandishi na wasanii ambao walioshiriki kwenye kampeni za Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Dk. John Pombe Magufuli ambapo aliwapongeza waandishi na wasanii kwa kazi nzuri waliyoifanya.
 Sehemu ya watu waliohudhuria.
 Wasanii wa bendi ya TOT

 Msanii wa Bongo movie JB akizungumza kuelezea furaha yao ya kuonana na Rais wa Jamhuri ya Muungano Dk. John Pombe Magufuli.
 Dereva mkongwe Ben Mugisha almaarufu 'Shemeji' akizungumza kwa niaba ya madereva walioshiriki kampeni.
 Kiongozi wa Bendi ya TOT Tumaini akizungumza kwa niaba ya wasanii wa muziki wa Dansi.

 Masanja wa Ze Komedi akizungumzia suala zima la maslahi ya wasanii ambapo alisema wasanii wanafanya kazi kubwa lakini maslahi madogo.
Msanii wa muziki wa kufoka foka Mwana FA akizungumzia suala la haki miliki za kazi za wasanii kuwa katika wizara ya viwanda na biashara na kutaka kama kuna uwezekano masuala yanayohusu sanaa yawe chini ya Wizara husika inayohusu sana.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.