Wednesday, February 17, 2016

CCM TAWI LA UINGEREZA WAPONGEZA SIKU 100 ZA UTENDAJI WA MAGUFULI

Tawi la Chama Cha Mapinduzi nchini Uingereza, wamepongeza juhudi za serikali ya awamu ya tano kwa uthubutu na kasi ya hali ya juu ya kurekebisha mfumo wa utendaji katika serikali ambapo umekuwa na uozo mwingi na wa muda mrefu uliopelekea wananchi hasa wa hali ya chini kukosa huduma za muhimu kutokana na watendaji wengi kufanya kazi kwa mazoea yaliyopelekea kuzorota kiufanisi.
WanaCCM hao wa Uingereza wamesema kuwa siku zote serikali ya CCM imekuwa ikipata lawama nyingi katika utendaji mbovu na hivyo kupelekea wananchi kukata tamaa na utendaji wa Serikali na Chama chenyewe ili hali ni baadhi tu ya watendaji wachache wabovu waliokuwa kwa makusudi mazima wanatenda kazi zao chini kiwango bila weledi ama kwa makusudi ili tu kuharibu sifa ya Chama Cha Mapinduzi.
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.