Monday, December 28, 2015

RAIS MAGUFULI AWAAPISHA LEO MAWAZIRI WAPYA ALIOWATEUA HIVI KARIBUNI

Mawaziri wapya wakisubiri kuapishwa leo Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mawaziri wapya wakiimba wimbo wa Taifa kabla ya kuapishwa leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Joseph Magufuli (kushoto) akimuapisha Mhe. Profesa Jumanne Maghembe (kulia) kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii,  leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Joseph Magufuli (kushoto) akimuapisha Mhe. Dkt. Joyce Ndalichako (kulia) kuwa  Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi. (Ni  baada ya kumteua kuwa Mbunge), leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Joseph Magufuli (kushoto) akimuapisha Mhe.  Dkt. Philip Mpango (kulia) kuwa  Waziri wa Fedha na Mipango (Ni baada ya kumteua  kuwa Mbunge), leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Joseph Magufuli (kushoto) akimuapisha Mhe.  Mhandisi Gerson Lwenge (kulia) kuwa  Waziri wa Maji na Umwagiliaji, leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Joseph Magufuli (kushoto) akimuapisha Mhe.   Profesa Makame Mbarawa (kulia) (amehamishwa kutoka Wizara ya Maji na Umwagiliaji) na kwenda Wizara ya Ujenzi, uchukuzi na Mawasiliano leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Joseph Magufuli (kushoto) akimuapisha Mhe.  Hamad Masauni (kulia) kuwa  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Joseph Magufuli (katikati)akiwa katika picha ya pamoja na Mawaziri wapya wanne na Manaibu Waziri leo Ikulu Jijini Dar es Salaam mara baada ya kuwaapisha. Wa pili kushoto mstari wa mbelel ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, wa pili kushoto ni Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majliwa.(Picha zote na Benedict Liwenga)

Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.