Thursday, December 17, 2015

KAMATI YA URATIBU YA SHIRIKISHO LA VYUO ELIMU YA JUU YAANZA VIKAO VYA SIKU MBILI

 Mwenyekiti wa Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu Zainab Abdallah (MNEC) akiongoza kikao cha Kamati ya Uratibu Taifa ya la Vyuo vya Elimu ya juu kilichofanyika kwenye ukumbi wa Sekretarieti, Makao Makuu ya CCM Ofisi Ndogo Lumumba jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu Zainab Abdallah (MNEC) akiongoza kikao cha Kamati ya Uratibu Taifa ya la Vyuo vya Elimu ya juu, kulia ni Katibu Mtendaji Ally S. Hapi

 Mwenyekiti wa Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu Zainab Abdallah (MNEC) akijadiliana jambo pamoja na  Daniel Zenda (katikati) na Ally S. Hapi wakati wa kikao cha Kamati ya Uratibu Taifa ya la Vyuo vya Elimu ya juu.
 Wajumbe wa kikao wakichambua mambo mbali mbali.

Kamati ya Uratibu taifa ya Shirikisho la Vyuo vya Elimu ya Juu leo imeanza kikao cha siku mbili kinachofanyika makao makuu ya CCM Ofisi Ndogo Lumumba jijini Dar es salaam
chini ya Mwenyekiti wake bi Zainab Abdallah(Mnec). Viongozi wengine wanaohudhuria kikao hicho ni Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho Ndg. Hamid Mhina (Mnec), Katibu Mtendaji Ally S. Hapi, Katibu mtendaji Daniel Zenda, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM taifa kutoka Shirikisho Joseph Chitinka,Katibu uchumi na Fedha Richard Luhende, katibu wa siasa na uenezi Fikiri Mzome na katibu wa uhamasishaji Mganwa Nzota.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.