Tuesday, December 8, 2015

HALMASHAURI YA LINDI VIJIJINI YAPATA MWENYEKITI


Mkuu wa Wilaya ya Lindi Ndugu Yahaya Nawanda akihutubia wakati wa ufunguzi wa kikao cha kwanza cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Lindi Vijijini ambapo aliwataka madiwani wao kuhakikisha suala la usafi linatiliwa mkazo kwenye maeneo yao.
 Baadhi ya madiwani wakisikiliza kwa makini.

 Mbunge wa Jimbo la Mtama Ndugu Nape Nnauye akipiga kura kumchagua Mwenyekiti wa Halmashauri ya Lindi Vijijini.
 Mbunge wa jimbo la Mtama ndugu Nape Nnauye (CCM) akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Mchinga ndugu Hamidu Bobali (CUF) walipokutana kwenye kika cha kwanza cha Halmashauri ya Lindi Vijijini ambapo pia ulifanyika uchaguzi wa Mwenyekiti wa Halmashauri na kuchagua kamati mbali mbali.
 
 Mwenyekiti aliyechaguliwa kuongoza Halmashauri ya Wilaya ya Lindi Vijijini Ndugu Matei B. Makwinya ambaye ni diwani wa kata ya Nyangao (CCM) akitoa salaam za shukrani kwa wajumbe wote waliompigia kura nyingi ambapo alipata kura 26 dhidi ya mpinzani wake aliyepata kura 17.
 Mbunge wa Mtama Ndugu Nape Nnauye (CCM) akimsikiliza diwani wa kata ya Sudi Bw. Ali Athumani Njale (CUF) ,mwingine kushoto ni Mzee Masoud Chitende mara baada ya zoezi la kupiga kura kumchagua Mwenyekiti wa Halmashauri kukamilika.

Madiwani wakiwa kwenye vazi rasmi wakati wa kikao
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.