LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Dec 4, 2015

COSATO CHUMI AMALIZA TATIZO LA VITANDA HOSPITAL YA MAFINGA MJINI


Pichani Mbunge wa jimbo la Mafinga mji ni Cotato chumi akimkabidhi msaada wa  vitanda ,magodoro pamoja na vifaa mbalimbali  kaimu mganga mkuu wa hospitali ya Mafinga dk Abdul Msuya juzi 
 baadhi ya waandishi wa habari wakifuatiliwa ugawaji wa vifaa hivyo wakati wa makabidhiano
 Mbunge wa Mafinga mjini Cosato Chumi akikabidhi vifaa hivyo kwa vitendo
Baadhi ya wadau na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi CCM walihudhulia tukio hilo 

TATIZO la upungufu wa vitanda katika wodi ya akina mama na watoto katika hospitali ya wilaya ya Mufindi mkoani Iringa ambalo kwa muda mrefu limekuwa chanzo cha msongamano na uwalazimu baadhi ya wagonjwa kulala sakafuni sasa limepatiwa ufumbuzi baada ya uongozi wa hospitali hiyo kupokea msaada wa vitanda na vifaa tiba kutoka kwa mdau wa maendeleo katika sekta ya afya.

mbunge wa Mafinga Mjini (CCM) Cosato Chumi alisema kuwa kwa muda mrefu hospitali hiyo ilikuwa ina upungufu wa vifaa mbalimbali ikiwemo vitanda hali iliyofanya kuandika maandiko mbalimbali kwa wahisani  wa nje ya nchi ili kuweza kumsaidia kupata vifaa hivyo .
  
Alisema kuwa umefika wakati sasa wadau mbalimbali, mifuko ya kijamii na makampuni kujenga utamaduni wa kusaidia watu wenye mahitaji mbalimbali wakiwemo watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu na wagonjwa hospitalini kwani kufanya hivyo ni sehemu ya kurudisha kile wanachokitapa kwa jamii.

“Unajua afya ni kila kitu katika maisha ya binadamu hivyo lazima nitekeleze ahadi zangu nilizotoa wakati wa kampeni na wanachi lazima tufanye kazi kwa kujituma ili tumuunge mkono rais wetu ambaye anania ya ya kutuletea maendeleo na kuwataka wadau mbalimbali kusaidia jamii zenye mahitaji na kuacha kutegemea serikali pekee “ alisema
Chumi aliwaomba wananchi wa jimbo hilo kuunga mkono kwa kufanya kazi kwa nguvu zote ili walete maendeleo kwa pamoja maana akifanya kazi pekee yake bila wao hawezi kuleta maendeleo pekee yake.
  
Msaada huo wa vitanda 16 na magodoro 11 na vitu mbalimbali umetolewa na taasisi binafsi inayojishughulisha na masuala ya afya ya nchini Astralia ijulikanayo kama “Rafiki Surgical Mission” kwa uratibu wa ofisi ya mbunge wa jimbo la Mafinga mjini 

Alisema kuwa msaada huo aliopatiwa  na rafiki zao hawajatoa hata senti tano bali huwa marafiki hao wanachangishana fedha na kununua vifaa hivyo na kisha kuvisafirisha mpaka bandari kavu ambapo hapo ndio hutumia garama kusafirisha vifaa hivyo mpaka sehemu husika

“Ndugu zangu nadhani kila mmoja alikuwa akifahamu machungu waliyokuwa wakipata mama zetu wanapokuja kujifungua kwa kukosa sehemu za kujifungulia lakini leo hii msaada huu utatusaidia sana na yoyote
atakayeguswa na anaweza kuja na kuchangia chochote maana mufindi ni yetu sote na mufindi itajegwa na wanamufindi wenyewe”alisema

Alisema jambo kubwa lilokuwa likimuumiza kicha kila kukicha ni tatizo la vifaa katika hospital, elimu  pamoja na tatizo la maji hivyo ni wakati wawanamafinga kushikana kwa pamoja katika kusumkuma mbele gurudumu la maendeleo ili kuendana na kauli mbiu ya sasa ya HAPA NI KAZI TU.

Akipokea msaada huo kaimu mganga mkuu wa hospitali ya Mafinga dk Abdul Msuya alisema kuwa msaada wa vitanda hivyo na magodoro na  vifaa mbalimbali utakuwa umemaliza kabisa tatizo la vitanda hospitalini hapo licha ya kukabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo zinaweza kumalizika endapo kutatokea mdau mwingine kuwasaidi Kwa upande wake katibu wa ccm wilaya ya Mufindi Jimsoni Muhagama
alimpongeza mbunge huyo kwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo huku akimwambia kuwa ni wakati wa kutekeleza kazi kwa vitendo na wala si maneno kwani wananchi wanapaswa kutatuliwa kero mbalimbali zinazowakabili badala ya kupiga porojo zisizo na msingi .

Mhagama alisema kuwa kila mmoja anapaswa kuwajibika ipasavyo katika nafasi yake kwani kasi anayokwenda nayo Rais John Magufuli si ya mchezo bali ni ya mchaka mchaka na ili nchi iweze kusimama katika mstari ulionyoka kila mmoja anapaswa kucheza wimbo wa mchaka mchaka

‘’Huuu si wakati lelemama huu sio wakati mchezo mchezo ni wakati wa uwajibikaji ,hakika Tanzania tumepata kiongozi mchapa kazi tazama sasa ni siku ya 27 nchi inaongozwa na watu wanne lakini kila sektaa imenyoka na mimi  nasemaa Magufuli wanyooshe tu kwa kuwa watu walikuwa wakifanya kazi kwa mazoeya bila ya kuangalia madhara wanayopata
watanzania swengi

Hata hivyo Mhgama alisema kuwa kwa kuwa kipindi cha muda mchache nchi inaongozwa na watu wachache na nchi imesimama haoni sababu ya kuwa na baraza kubwa la mawaziri bali Rais Magufuli achague baraza dogo kama
la watu 10 ili kupunguza mzigo kwa serekali yake ya kuwa na mawziri wengi wasiokuwa na tija  .

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages