DK TULIA ACKSON NDIE NAIBU SPIKA WA BUNGE LA 11 LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

 Dk. Tulia Ackson amechaguliwa kuwa Naibu Spika wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo ameshinda kwa kura 250 sawa na asilimia 71.2% ambapo mshindani wake Mhe. Magdalena Sakaya alipata kura 101.

Idadi ya Wabunge inayotakiwa ni 394, waliosajiliwa 369, akidi ni 184 na waliohudhuria ni 351 na hakukuwa na kura iliyoharibika.