Wednesday, October 7, 2015

MAGUFULI AZIDI KUIHAKIKISHIA CCM USHINDI MKOANI KILIMANJARO


Na Mwandishi Wetu, Kilimanjaro
Mgombea uraia kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli leo ameutikisa Mkoa wa Kilimanjaro na viunga vyake.
Dk. Magufuli ambaye aliwasili mkoani hapa akitokea Mkoa wa Arusha katika kampeni za kuomba ridhaa ya kuchaguliwa kuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mgombea huyo wa urais amewasili mkoani hapa ukiwa ni mkoa wake wa 22 ambapo alitikisa kwa kufanya mikutano yake kwenye majimbo ya Siha, Hai na Moshi Mjini ambapo mamia ya wanachi walijitokeza kumsikiliza.
Akiwa Moshi Mjini, Dk. Magufuli amesema amejipanga kuwatumikia Watanzania kwa kuwapa utumishi uliotukuka pindi watakaopomchagua kuongoza nchi.
 Mgombea urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa manispaa ya Moshi mjini kwenye mkutano wa kampeni za Urais uliofanyika kwenye uwanja wa Mashujaa, Moshi mjini mkoani Kilimanjaro.
 Umati wa wakazi wa manispaa ya Moshi mjini wakimsikiliza Mgombea urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye viwanja vya Mashujaa.

 Msanii wa muziki wa kufoka foka Chid Benz akitumbuiza kwenye  mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika kwenye viwanja vya Mashujaa.

 Ali Kiba akishambulia jukwaa pamoja na wacheza show wake

 Mgombea ubunge jimbo la Moshi mjini Davis Mosha akicheza pamoja na Yamoto Band.

 Wakazi wa manispaa ya Moshi mjini wakiwa na shangwe ya chama chao cha CCM wakati wa mkutano wa kampeni za kumnadi mgombea urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli.
 Wasanii wa muziki wa kizazi kipya wakiimba nyimbo maalum kwa ajili ya Mgombea urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli.
 Dk. Emmanuel Nchimbi akihutubia wakazi wa Manispaa ya Moshi mjini ambapo aliwaeleza wananchi hao kuwa Mgombea urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli ni mtu sahihi kwa wakati huu ambao Taifa linahitaji kiongozi shupavu.
 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi na mjumbe wa kamati kuu ya CCM Taifa Ndugu Abdallah Bulembo akionyesha wananchi wa manispaa ya Moshi mjini namna watakavyopigia CCM kura.
 Wazee wa CCM Moshi mjini waliojitokeza kwenye mkutano wa kumnadi Mgombea urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli
 Umati huu unaonyesha namna gani Chama Cha Mapinduzi kinakubalika Moshi mjini.
 Mgombea urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akimtambulisha mgombea wa ubunge jimbo la Moshi mjini Mhe. Davis Mosha.
 Msanii wa muziki wa bongo flava Juma Nature akitumbuiza kwenye mkutano wa kampeni za CCM za kumnadi Mgombea urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli uliofanyika viwanja vya Mashujaa.
Wana CCM wakiwa wanarudi kwa shangwe mara baada ya mkutano wa kampeni za kumnadi Mgombea urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli kumalizika salama.
 Mgombea urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali Mrisho Sarakikya wakati wa mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika kwenye viwanja vya Ngaraselo,Arumeru Mashariki.
 Mgombea urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akimsikiliza mgombea wa ubunge jimbo la Arumeru Mashariki Ndugu John Daniel Pallangyo kabla ya kuhutubia wananchi waliojitokeza kwa wingi kwenye uwanja wa Ngaraselo.
 Uwanja wa Ngaraselo ulivyofurika.
 Mgombea urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akimnadi mgombea ubunge jimbo la Arumeru Mashariki Ndugu John Daniel Pallangyo kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye viwanja vya Ngaraselo, Arumeru Mashariki.
 Mgombea urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa jimbo la Siha kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika uwanja wa CCM wilaya ya Siha.
 Wakazi wa Sanya Juu wakimsikiliza Mgombea urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli alipokuwa akihutubia kwenye uwanja wa CCM wilaya.
 Mgombea ubunge jimbo la Siha Ndugu Aggrey Mwanri akihutubia wakazi waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa CCM uliofanyika viwanja vya CCM wilaya ambapo Mgombea urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli alihutubia pia.


 Mgombea urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa wilaya ya Hai kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika viwanja vya Snow View ,Boma Ng'ombe ambapo aliwaambia uchumi wa Tanzania utakuwa kama viwanda vitakuwa vingi na kusimamiwa vizuri.
 Mgombea urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiruka juu kwa mtindo wa kimaasai mara baada ya kukabidhiwa rungu na wamasai wa vijiji jirani na uwanja wa ndege wa KIA.
 Mgombea urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiondoka kwenye viwanja vya snow View Boma Ng'ombe mara baada ya kumaliza kuhutubia.
Mgombea urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akimnadi Moshi vijijini Dkt Cyril Chami kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika Uru Shimbwe.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
Share:

KUCHAGUA LUGHA

IDADI YA WATU AMBAO HUTEMBELEA BLOGU HII

KUMBUKUMBU ZA POSTI ZOTE

JISAJILI UPATE TAARIFA KWA EMAIL

Jisajili ili upate taarifa kwa email

Google+ Followers

Powered by Blogger.