Wednesday, September 30, 2015

WARIOBA AMPONGEZA MAGUFULI KWA KUHUBIRI AMANI

 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwasili kwenye uwanja wa jamhuri tayari kuhutubia wakazi wa Dodoma mjini.
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Dodoma mjini waliofurika kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika ndani ya uwanja wa Jamhuri mjini hapo.
 Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba akielezea umuhimu wa amani katika Taifa letu na kusema kuna umuhimu wananchi kujifunza historia kabla ya kuwania nafasi mbali mbali za uongozi kwani itasaidia kutunza na kuilinda misingi iliyowekwa na waasisi wa  Taifa hili.
Warioba alimpongeza sana mgombea wa urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli kwa kuhubiri amani katika kila mkutano wake wa kampeni kitu ambacho kinasaidia sana kuwakumbusha wananchi wa Tanzania kudumisha na kuitunza amani kati yetu.
 Mgombea Ubunge jimbo la Dodoma mjini akimuelezea Mgombea wa Urais wa CCM Dk. John Pombe Magufuli changamoto mbali mbali za Dodoma mjini kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri mjini hapo.
 Mgombea ubunge wa jimbo la Dodoma mjini Ndugu Anthony Mavunde akihutubia wakazi wa Dodoma mjini mbele ya mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli kwenye uwanja wa Jamhuri mjini hapo.
 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe.Abdalla Bulembo akihutubia wakazi wa Dodoma mjini kwenye mkutano wa kampeni za kumnadi mgombea urais wa CCM Dk. John Pombe Magufuli kwenye uwanja wa Jamhuri mjini hapo.
 Mgombea wa Ubunge jimbo la Dodoma mjini Anthony Mavunde akicheza muziki wa vijana wa Temeke mtindo maarufu unaojulikana kama mapanga shaa sambamba na Chegge na Temba .
 Mtayarishaji wa Muziki wa Kizazi kipya P Funky Majani akiwasalimu wakazi wa Dodoma na kuwaambia kila mmoja wao ana jukumu la kumpigia kura mgombea wa Chama Cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli.
 Ali Kiba katikati akiimba na kucheza pamoja na wacheza show wake kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofnyika kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.
 Msanii Tunda Man akitumbuiza kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.
 Wahamasishaji wakicheza wakati wa mkutano wa kampeni za CCM.
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli (wa pili kushoto)akiwa jukwaani pamoja na viongozi wengine ,Mawaziri Wakuu wastaafu Jaji Joseph  Warioba, Mzee Samuel Malecela, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma Adam Kimbisa na Mgombea Ubunge wa jimbo la Dodoma mjini Ndugu Anthony Mavunde.
Mgombea Ubunge wa jimbo la Mtera Ndugu Livingstone Lusinde akipiga push up kama ishara ya kumuunga mkono mgombea urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.
 Umati wa wakazi wa Kibaigwa mkoani Dodoma wakimsikiliza mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika kwenye uwanja wa shule ya msingi Kibaigwa maarufu kama Kibaigwa Mama.
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Kibaigwa kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Kibaigwa.
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Mpwapwa kwenye uwanja wa Chuo cha Ualimu Mpwapwa.
 Mgombea Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akimkabidhi ilani ya uchaguzi ya CCM Mgombea wa Ubunge jimbo la Kongwa Ndugu Job Ndugai kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye viwanja vya CCM Kongwa.
 Mgombea Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu wa Zamani Jaji Joseph Warioba.
 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma Alhaji Adam Kimbisa akihutubia wakazi wa Kibaigwa kwenye mkutano wa kampeni za CCM kumnadi mgombea wa urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
Share:

KUCHAGUA LUGHA

IDADI YA WATU AMBAO HUTEMBELEA BLOGU HII

KUMBUKUMBU ZA POSTI ZOTE

JISAJILI UPATE TAARIFA KWA EMAIL

Jisajili ili upate taarifa kwa email

Google+ Followers

Powered by Blogger.