Monday, September 7, 2015

UONGOZI WA CHADEMA WILAYA YA KILOSA WAJIUNGA NA CCM

Viongozi watatu wa Chadema wilaya ya Kilosa na mwanachama mmoja wametangaza kujiunga rasmi na CCM baada ya kuchoshwa na siasa za Chadema ambazo wameona hazina haki.
 Viongozi hao waliohamia CCM ni aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Kilosa Ndugu Selemani Simba, Katibu wa Chadema wilaya hiyo Ndugu Ibrahim Abdallah Selemani, aliyekuwa Katibu wa Jimbo la Kilosa Kati Mussa Ngongo na aliyejitambulisha kama mwanachama kiherehere wa Chadema Bi.Oliver Mollel.
Viongozi hao walitangaza kukihama chama cha Chadema kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni za CCM mbele ya mgombea wa urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli kwenye uwanja wa Kilosa town.
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.