URAIS CCM: VIKAO VYAFANYIKA LEO, MKUTANO MKUU KESHO


 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari nje ya ukumbi wa NEC,Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma. 
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi aliwaeleza waandishi wa habari kuwa vikao vyote vitafanyika leo kikiwemo cha Kamati ya Usalama na Maadili pamoja na vikao vya mchujo wa wagombea kuanzia watano(5) mpaka kupata watatu (3) ,mgombea wa Urais Zanzibar kisha kesho tarehe 11 Julai utafanyika mkutano mkuu wa CCM ambao atapatikana mgombea mmoja wa CCM kwa nafasi ya Urais.


Waandishi wa habari wakichukua taarifa za vikao vitakavyofanyika leo mjini Dodoma kutoka kwa msemaji wa Chama Cha Mapinduzi, Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye nje ya ukumbi wa NEC mjini Dodoma.