UANDIKISHAJI WANANCHI BVR KUANZA LEO DAR ES SALAAM

Kazi ya kuandikisha wananchi kwenye daftari la kudumu la wapigakura inaanza leo katika mkoa wa Dar es Salaam, ewe mwananchi hii ni fursa yako ili uweze kupata haki ya kuwa mpigakura katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu wa 2015. Uandikishaji huu ni katika mfumo unaoelezwa kuwa ni wa kisasa wa BVR.