BREAKING NEWS

Post Top Ad

Your Ad Spot

Sunday, July 12, 2015

MKUTANO MKUU MAALUM WA UCHAGUZI WA MGOMBEA WA URAIS KWA TIKETI YA CCM WAFANYIKA USIKU HUU MJINI DODOMA

 Mmoja wa waomba kugombea urais kwa tiketi ya CCM, waliotinga tatu bora, Dk. John Magufuli akingia katika ukumbi wa Kisasa wa mikutano wa CCM, mjini Dodoma, wakati wa mkutano mkuu wa CCM, uliofanya uchaguzi leo usiku wa kupata mgombea mmoja wa urais kwa tiketi ya CCM katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu. Picha zote na Bashir Nkoromo na Adam Mzee
Mmoja wa waomba kugombea urais kwa tiketi ya CCM, waliotinga tatu bora, Dk. John Magufuli akiwasalimia wajumbe na waalikwa baada ya kuingia katika ukumbi wa Kisasa wa mikutano wa CCM, mjini Dodoma, wakati wa mkutano mkuu wa CCM, uliofanya uchaguzi leo usiku wa kupata mgombea mmoja wa urais kwa tiketi ya CCM katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu.
Mmoja wa waomba kugombea urais kwa tiketi ya CCM, waliotinga tatu bora, Dk. John Magufuli akicheza jukwaani huku Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akimwangalia, baada ya kuingia katika ukumbi wa Kisasa wa mikutano wa CCM, mjini Dodoma, wakati wa mkutano mkuu wa CCM, uliofanya uchaguzi leo usiku wa kupata mgombea mmoja wa urais kwa tiketi ya CCM katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu
Mmoja wa waomba kugombea urais kwa tiketi ya CCM, waliotinga tatu bora, Dk. John Magufuli akijitambulisha jukwaani kwa wajumbe na wageni waalikwa baada ya kuingia katika ukumbi wa Kisasa wa mikutano wa CCM, mjini Dodoma, wakati wa mkutano mkuu wa CCM, uliofanya uchaguzi leo usiku wa kupata mgombea mmoja wa urais kwa tiketi ya CCM katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu
Mmoja wa waomba kugombea urais kwa tiketi ya CCM, waliotinga tatu bora, Dk. John Magufuli akisalimiwa na Meya wa Manispaa ya Ilala, Dar es Salaam, Jery Silaa, baada ya kuingia katika ukumbi wa Kisasa wa mikutano wa CCM, mjini Dodoma, wakati wa mkutano mkuu wa CCM, uliofanya uchaguzi leo usiku wa kupata mgombea mmoja wa urais kwa tiketi ya CCM katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akifurahiwa na wajumbe wa mkutano huo, wakati akihamasisha jukwaani.
Huyu ndiyo, Dk. John Magufuli, akiwa mwenye sura ya furaha wakati yupo ukumbini, wakati wa mkutano huo.
Familia au watoto wa Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete ni miongoni mwa wageni waalikwa waliohudhuria mkutano huo.
Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete akiwasili ukumbini huku akiwa amejawa na furaha wakati wa mkutano huo.
Baadhi ya wake wa viongozi wakiwa ukumbini wakati wa mkutano huo.
Aliyekuwa muomba kuteuliwa na CCM kuwania Urais, Waziri Mkuu wa zamani, Edrward Lowassa, akimsikiliza Mbunge wa Kigoma  mjini ambaye anaelezwa kuwa mdau wake wa karibu, Peter Serukamba, wakati akimweleza jambo wakati wa mkutano huo.
Aliyekuwa mwomba ridhaa ya CCM kuwania Urais, Januari Makamba ambaye pia alifanikiwa kuingia tano bora, akimsalimia mke wa Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi, Siti Mwinyi, wakati wa mkutano huo.
Wajume wakifuatilia hatua kwa hatua, mambo yalivyokuwa yakijiri wakati wa mkutano huo.
Mmoja wa waomba kugombea urais kwa tiketi ya CCM, waliotinga tatu bora, Dk. John Magufuli akiomba kura kwa wajumbe wakati wa mkutano huo.
Mmoja wa waomba kugombea urais kwa tiketi ya CCM, waliotinga tatu bora, Dk. John Magufuli akiomba baraka kwa Mama Fatma Abeid Amani Karume, wakati wa mkutano huo.

 KINANA AMKABILI LOWASSA
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akizungumza na aliyekuwa muomba ridhaa ya CCM kuwania Urais, Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa, baada ya kumfuata alikokuwa ameketi wakati wa mkutano huo.
Mmoja wa waomba kugombea urais kwa tiketi ya CCM, waliotinga tatu bora, Dk. John Magufuli akimsalimia Mama Anne Kilango Malecela, ukumbini.
Mmoja wa waomba kugombea urais kwa tiketi ya CCM, waliotinga tatu bora, Dk. John Magufuli akiwasalimia watoto wa Rais Jakaya Kikwete, ukumbini wakati wa mkutano huo.
Waziri Mkuu wa zamani, Jaji Mstaafu, Joseph Warioba akimsalimia Lowassa, wakati wa mkutano huo
Jaji Mstaafu Joseph Warioba akizungumza na Lowassa
Rais Mstaafu, Ali Hassani Mwinyi akiingia ukumbini, wakati wa mkutano huo
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akimsalimia Rais Mstaafu na Mwenyekiti mstaafu wa CCM, Benjamin Mkapa, baada ya kuwasili ukumbini.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiwasalimia wajumbe na wageni waalikwa baada ya kuwasili kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete akiwa na viongozi wa meza kuu baada ya kuwasili ukumbini. Kutoka kushoto ni Makamu wa Pili wa Rais wa zanzibar, Balozi Ali Seif Idi, Makamu wa Rais Dk. Mohammed Bilal,Makamu Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein na kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.
Mmoja wa waomba ridhaa ya CCM kugombea Urais  Balozi Amina Salim Ally, akisindikizwa na wapambe kuomba kura kwa wajumbe.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akijadili jambo na Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana (Jembe), wakati wa mkutano huo.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akihamasisha wajumbe wakati wa mkutano huo.
Wazee wastaafu, Ali Hassani Mwinyi, Amani Abeid Karume, Pius Msekwa na Dk. Salim ahmed Salim wakiwa ukumbini wakati wa mkutano huo.
Mwimbaji wa TOT, aliyepewa 'viatu' vya aliyekuwa Mkurugenzi wa kundi hilo la CCM, John Komba, Komba Jr, akiongoza kuimba wimbo wa 'CCM mbele kwa mbele' wakati wa mkutano huo.
Abdul Misambano aliyeimba wimbo huo na Marehemu John Komba akiimba sehemu ya wimbo huo wa CCM mbele kwa mbele.
Wajumbe wakihamasika na mabango ya mikoa yao mbele ya jukwaa kuu wakati wa mkutano huo
"Kina mama ni Wale wale.. Mnasemajeee?" Malkia wa mipasho Khadija Kopa, akihanikiza wakati akiimba sehemu ya wimbo wa CCM mbele kwa mbele wakati wa mkutano huo.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akitoa maneno ya utangulizi wakati akimkaribisha Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete kufungua mkutano huo.
Wajumbe wakiwa wamesheheni ukumbini.
Baadhi ya Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao Tanzania, wakiwa ukumbini wakati wa mkutano huo.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiongoza wajumbe kusimama kwa dakika chache kuwakumbuka wajumbe wa mkutano huo, akiwemo Marehemu John Komba wakati wa mkutano huo.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akizungumza wakati wa kufungua mkutano huo.
"Wagombea hawa watatu tuliowaletea wote wana sifa za kuwa Rais, mkimchagua mmoja wapo atakuwa mchapakazi, maana tumewachuja vya kutosha kuhakikisha wanazo sifa za kutosha kuwa Rais.." Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akisisitiza hilo wakati akiufungua mkutano huo.
aadhi ya wajumbe kutoka Dar es Salaam, wakiwa ukumbini wakati wa mkutano huo.

ZAMU YA WAGOMBEA KUJIELEZA
Muomba kuchaguliwa kuwania Urais kwa tiketi ya CCM, Amina Salum Ally, akijieleza na kuwaomba kura kwa wajumbe wakati wa mkutano huo.
Muomba kuchaguliwa kuwania Urais kwa tiketi ya CCM, Dk. Asha-Rose Migiro, akijieleza na kuwaomba kura kwa wajumbe wakati wa mkutano huo.
Muomba kuchaguliwa kuwania Urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Pombe Magufuli, akijieleza na kuwaomba kura kwa wajumbe wakati wa mkutano huo.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akitangaza kufanyika uchaguzi.
Baadhi ya Wazee Maarufu wakiwa kwenye mkutano huo
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Adam Bimbisa (wapili kushoto) akijadili jambo na Kijana, Sambara wakati wa mkutano huo.
Mjumbe wa mkutano huo, Profesa Anna Tibaijuka akijadili jambo na mjumbe mwenzake wakati wa mkutano huo.
Makatibu wa CCM wa wilaya mbalimbali wakiwa na masanduku ya kura baada ya kura kupigwa
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa mkutanoni
Muomba kuchaguliwa kuwania Urais kwa tiketi ya CCM, Dk. asha Rose Migiro akiwa mwenye furaha wakati wa mkutano huo.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akipiga kura yake wakati wa mkutano huo.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akipiga kura yake wakati wa mkutano huo
Makamu Mwenyekiti wa CCM, Philip Mangula akipiga kura yake wakati wa mkutano huo. Hadi tunakwenda mitamboni matokeo yalikuwa hayajatangazwa. Picha zote na Bashir Nkoromo na Adam Mzee.

No comments:

Post a Comment

Mdau, andikamaoni yako hapa yasaidie kujua wewe unafikiri nini kuhusu posti hii. Tafdhali, Maoni yako yasiwe ya uchochezi wa aina yoyote.. Mawasiliano yetu:- simu +255 (0) 712 498008, Email: nkoromo@gmail.com.
Bashir Nkoromo
Msimamizi Mkuu, Blog ya Taifa ya CCM.

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages