Friday, July 10, 2015

KAMATI KUU YA CCM YAKUTANA JIONI HII KUTEUA MAJINA MATANO YA WAOMBA KUGOMBEA URAIS KWA TIKETI YA CCM

 Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiwa amewasili ukumbi tayari kwa kuendesha Kikao Cha Kamati Kuu ya CCM, cha kuteua wagombea watano, kwa ajili ya kupelekwa katika Kikao Cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM NEC,ambacho nacho kitapitisha majina matatu kwa ajili ya kwenda kupigiwa kura katika mkutano mkuu wa Taifa ili kupata mgombea mmoja atakayepeperusha bendera ya CCM katika kuwania Urais katika uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwishoni mwa mwaka huu. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein na Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Philip Mangula na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akifungua kikao hicho
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akitoa maneno ya utangulizi kabla ya Rais Kikwete kufungua kikao hicho leo jioni.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimshauri jambo, Mwenyeki wa CCM, Abdulrahman Kinana wakati wa kikao hicho
  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimshauri jambo, Mwenyeki wa CCM, Abdulrahman Kinana wakati wa kikao hicho
 Spika wa lililokuwa Baraza la wawakilishi, Pandu Ameir Kificho na Spika wa Bunge Anna Makinda wakisubiri kwa hamu kuanzakwa kikao hicho.
 Wajumbe waalikwa katika Kikao hicho, kutoka Baraza la Ushauri la Wazee wastafu wa CCM, wakiwa kwenye kikao hicho. Kutoka Kushoto ni Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu Benjamin Mkapa, Makamu Mwenyekiti wa CCM Mstaafu Pius Msekwa na Waziri Mkuuwa zamani, Cleopa Msuya.
 Mzee Mwinyi akifurahia jambo  na Mzee Mkapa kabla ya kikao kuanza
 Mzee Msekwa na Mzee Msuya
 Mgombea Urais, Makamu Wa Rais, Dk. Muhammed Gharib Bilal akisalimia wajumbe kwa unyenyekevu alipoingia ukumbini. Baadaye alitolewa nje ya ukumbi wakati kikao kilipoanza
 Makame Mbarawa na Dk. Hussein Mwinyi kikaoni
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akijadili jambo la Mjumbe mwenzake Adam Kimbisa
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM,Emmanuel Nchimbi akiwasalimia wajumbe wenzake.
 Mjumbe wa Kamati Kuu, Rais mstaafu wa Zanzibar,  Aman Abeid Karume akisalimia wajumbe
 Wajumbe wakiwa wameketi ukumbini
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akijadili jambo na mjumbe mwenzake wa Kamati Kuu ya CCM, Zakia Meghji
 JK alipokuwa akiwasili ukumbini
 JK baada ya kuketi ukumbini
 Katibu Mkuu wa CCM akimkaribisha Mwenyekiti wa CCM Jakaya Kikwete kufungua kikao
Kikao kikiendelea
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.